RAIS MAGUFULI ATEUA MWENYEKITI WA BARAZA LA USHINDANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 18 Agosti, 2017 amemteua Mhe. Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani (Fair Competition Tribunal - FCT).

Mhe. Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhe. Jaji Zainab Goronya Muruke ambaye amemaliza muda wake.

Kabla ya uteuzi huu Mhe.  Jaji Barke Mbaraka Aboud Sehel alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara.

Wajumbe wa Baraza la Ushindani ni;
  1.     Mustafa Siyani
  2.     Donald L. Chidowu
  3.     Susana Mkapa
  4.     Bibi Bitamo Kasuku Phillip
  5.     Yose Joseph Mlyambina
  6.     Dkt. Theodora Mwenegoha
Uteuzi huu umeanza  tarehe 18 Agosti, 2017

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
18 Agosti, 2017

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post