RAIS MAGUFULI AMPONGEZA PAUL KAGAME KUCHAGULIWA TENA KUWA RAIS WA RWANDA

Rais wa Rwanda Paul Kagame ametangazwa mshindi wa Urais wa nchi hiyo baada ya kushinda katika uchaguzi Mkuu uliofanyika August 4, 2017 na kumrudisha madarakani kwa muhula wa tatu.


Baada ya ushindi huo Rais wa Tanzania John Magufuli ametumia ukurasa wake twitter kumtumia salamu za pongeni Rais Kagame.

”Nakupongeza Mhe. Paul Kagame kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Rwanda kwa kipindi kingine. Kwa niaba ya Watanzania wote nakutakia mafanikio mema.

"Tutaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano na uhusiano kati ya nchi zetu hususani biashara na maisha ya wananchi wetu. Hongera Wanyarwanda. "Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post