NIC BANK YAKABIDHI MAGARI MATATU KATI YA SITA KWA MTEJA WAKE KAMA MKOPO


Meneja mahusiano kwa wateja wakubwa wa benki ya NIC Tanzania, Woinde Murro(kulia) akizungumza jambo na mmoja wa wateja waliofika kwaajili ya kukabidhiwa magari makubwa ikiwa awamu ya kwanza ya mkopo wa Magari Sita ambapo leo amepokea magari matatu na matela matatu.
Meneja mahusiano kwa wateja wakubwa wa benki ya NIC Tanzania, Woinde Murro(kulia) akimkabidhi funguo Mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya Simeta, Bw.Zainul Dossa(kushoto) za magari matatu waliyokopeshwa na Benki ya NIC
Meneja Uendeshaji kutoka Kampuni ya Usafirishaji ya Simera, Bw. Arif akiwasha moja ya gari mara baada ya Benki ya NIC kukopesha magari sita kwenye kampuni ya Usafirishaji ya Simera leo jijini Dar es Salaam.

Magari matatu kati ya sita yalikabidhiwa na benki ya NIC kama mkopo kwa mteja wao

Leo benki ya NIC imekabidhi magari makubwa matatu na matela yake kati ya magari sita ambayo yamekabidhiwa kama mkopo kwa Mteja wao Simera. Makabidhiano ya Magari hayo yamefanyika katika Ofisi za FAW zilizopo Barabara ya Nyerere jijini Dar Es Salaam.

Mkurugenzi wa kampuni ya Usafirishaji ya Simera, Bw.Zainul Dossa amepokea magari hayo kati ya sita waliyokopeshwa na Benki ya NIC mapema leo huku magari mengine matatu yatakabidhiwa hivi karibuni.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527