MWALIMU AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUFANYA MAPENZI NA MWANAFUNZI WAKE

Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Kata ya Igurubi, Maganga Ngassa (35) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Igunga mkoani Tabora kwa tuhuma ya kufanya mapenzi na mwanafunzi wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari kidato cha nne, Kata ya Mwisi wilayani hapa.


Mwendesha Mashitaka wa Polisi Igunga, Elimajid Kweyamba alidai mbele ya Hakimu Juhudi Mdonya, kwamba Julai 25, mwaka huu saa 9 alasiri katika nyumba ya kulala wageni ijulikanayo kwa jina la Forest au Chacha iliyoko Mtaa wa Mwayunge mjini Igunga, kinyume na sheria za nchi, Ngassa alifanya mapenzi na mwanafunzi mwenye umri wa miaka 17 anayesoma shule ya sekondari iliyoko Kata ya Mwisi kidato cha nne (jina linahifadhiwa). 


Mshitakiwa alikana kutenda kosa hilo ambapo kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 18, mwaka huu itakapotajwa tena.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post