MBUNGE WA CHADEMA ESTER BULAYA AKAMATWA NA POLISITaarifa zilizonifikia kutoka Bunda katika Mkoa wa Mara zinasema kuwa Mbunge wa Bunda Mjini Ester Bulaya amekamatwa na Jeshi la Polisi Mara kwa agizo la Mkuu wa Wilaya Tarime Glorious Luoga.

Bulaya amekamatwa na jeshi la Polisi akiwa katika Hotel ya Kifa Best Point Wilayani Tarime akidaiwa kujiandaa kutaka kufanya mkusanyiko kinyume cha sheria.

Kamanda wa polisi Tarime/Rorya Kamishina Msaidizi Mwandamizi Henry Mwaibambe amesema wabunge Bulaya na John Heche hawatakiwi kujumuika kwenye mkutano wa mbunge wa jimbo ka Tarime.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post