KAULI YA HUMPREY POLEPOLE BAADA YA KUAMBIWA VITU VYA NAPE NNAUYE VINAMPWAYA

Kupitia kwenye account yake ya twitter Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi CCM, Humphrey Polepole ametoa majibu kwa Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa akimwambia kuwa hatokuwa tena Mbunge baada ya Awamu hii.

Hatua hiyo ya Polepole imekuja baada ya kuambiwa na Mbunge Msigwa kuwa viatu vya Nape havimtoshi kupitia twitter ambapo aliandika; "Kitendo cha Msukuma kumkumbuka Nape , ni ujumbe tosha Kuwa Viatu vya Nape vinampwaya POLEPOLE!"
Kitendo cha Msukuma kumkumbuka Nape , ni ujumbe tosha Kuwa Viatu vya Nape vibampwaya POLEPOLE!

Baada ya ujumbe huo naye Polepole kupitia twitter aliandika; "Kitu kimoja nakuahidi, hii ni term yako ya mwisho, tunakurudisha kufanya kazi ya Uchungaji maana naona mchungaji anajichanganya na mbuzi."
Kitu kimoja nakuahidi, hii ni term yako ya mwisho, tunakurudisha kufanya kazi ya Uchungaji maana naona mchungaji anajichanganya na mbuzi https://twitter.com/MsigwaPeter/status/899874095743070208 


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post