WAZIRI MKUU : HALI YA CHAKULA HAIRIDHISHI TANZANIA

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema hali ya chakula nchini kwa sasa hairidhishi.


Majaliwa ametoa kauli hiyo leo (Julai 5,2017) alipohitimisha shughuli za mkutano wa saba wa Bunge la 11 mjini Dodoma.


Akizungumzia hali ya chakula nchini, Waziri Mkuu amesema bado kuna maeneo yenye upungufu wa chakula.


"Hali ya chakula si ya kuridhisha sana, bado kuna maeneo yenye upungufu wa chakula," amesema.


Majaliwa amesema hata hivyo, kuna maeneo yaliyopata mvua nyingi na chakula cha kutosha.


"Hii ni kutokana na mazao ya chakula kuanza kukomaa katika maeneo hayo. Pia, baadhi ya wakulima kuanza kuvuna mazao yao,” amesema.


Waziri Mkuu amesema kwa baadhi ya maeneo mazao ya chakula na hasa mahindi yameanza kushuka bei katika masoko.


Amesema licha ya upungufu wa chakula katika nchi zinazoizunguka Tanzania, Serikali imepiga marufuku usafirishaji wa mahindi nje ya nchi bila kibali.


Pia, ameagiza mazao kuongezwa thamani badala ya kusafirishwa yakiwa ghafi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post