TCU YABADILI MFUMO WA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU MWAKA WA MASOMO 2017 / 2018

Profesa Eleuther Mwageni.

Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imesema maombi ya kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka wa masomo 2017/2018 yatatumwa moja kwa moja vyuoni.

Akizungumza leo Julai 20, Kaimu Katibu Mtendaji TCU, Profesa Eleuther Mwageni amesema hawatapokea maombi ya kujiunga na vyuo vikuu kama ilivyokuwa hapo mwanzo. 

Maombi ya kujiunga na elimu ya juu yataanza kupokelewa rasmi Julai 22 kwenye vyuo vyote vya elimu ya juu nchini.

“Wanafunzi wenye sifa za kujiunga na vyuo vikuu wasisite kuchagua vyuo wanavyovipenda na kuhakikisha wanakuwa makini na programu zilizowekwa na vyuo iwapo zinatambuliwa na Tume,” Amesema.

Amesema TCU haitatoza ada yoyote ya udahili kwa waombaji.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post