SUMAYE: HATUKO TAYARI KUZIBWA MIDOMO NA SERIKALI

Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani na Mjumbe wa Halmashauri Kuu Chadema, Frederick Sumaye amesema kuwa licha ya kukatazwa wasizungumze masuala ya kisiasa, lakini hawatanyamaza.


Akizungumza na vyombo vya habari leo, Sumaye amesema kuwa wataendelea kufanya kazi kwa niaba ya wananchi ambao wana imani nao.


Amesema nchi kwa sasa inakazana kujenga mfumo wa demokrasia kandamizi ambayo kwa kiasi kikubwa inarudisha nyuma maendeleo.

"Viongozi wa upinzani wamekuwa wakikamatwa, wanawekwa rumande, wanatishwa lengo ni kudhoofisha upinzani," amesema Sumaye.


Amesema licha ya juhudi hizo za kuwarubuni baadhi ya viongozi wakiwamo madiwani wachache, hawatadhoofika na wataendelea kufanya Kazi.


Sumaye amesema kwamba wanataka kujenga upinzani wa kweli wenye lengo la kusaidia wananchi.


Amesema katika kulihakikisha hilo hadi kufikia mwaka 2018 hakutakuwa na kijiji, mtaa utakaokuwa hauna tawi la Chadema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527