POLISI DUBAI WAZINDUA GARI LISILOTUMIA DEREVA KWA AJILI YA KUKABILIANA NA MATUKIO YA KIHALIFU KWA HARAKA

Polisi wa Dubai wameanzisha program maalum kutumia magari yasiyokuwa na dereva na yenye kamera maalum kufanya doria kwenye miji mikubwa na sehemu zenye mikusanyiko ili kukabiliana na matukio ya kihalifu kwa haraka.

Program hiyo itatumia magari hayo yenye uwezo wa kukimbia kwa kasi ya 9.3 mph, kutambua sura za wahalifu wanaotafutwa, kamera aina ya drone inayoweza kumfuatilia mhalifu alipokimbilia na kutambua namba za magari yaliyoibiwa.

Magari hayo yametengenezwa kwa teknolojia ya kisasa inayoweza kunasa matukio yasiyokuwa ya kawaida kutoka umbali wa futi 330 na kutuma taarifa kupitia simu za mkononi kwa Maafisa wa Polisi walio kwenye vituo vya Polisi vilivyo karibu.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post