Picha: MTOTO WA MIAKA 8 ACHOMWA KWA KIJIKO CHA MOTO NA MAMA WA KAMBO GEITA


Jeraha la masikioni ambalo mtoto huyo amechomwa na mama wa kambo.

Mtoto huyo akionesha majeraha ya kuchomwa na kijiko ambacho kilikuwa kimepashwa moto maeneo ya miguuni.

Bi,Benitha Agustine ambaye ni mama wa Kambo wa mtoto ambaye amekuwa akimfanyia ukatili.

Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Esnath Magoti akizungumzia matukio ya ukatili ambayo yapo Mkoani Humo.

***


Hata hivyo kutokana na juhudi za utoaji wa elimu juu ya watu kuachana na vitendo vya ukatili hali bado sio shwari ambapo kwenye mtaa wa Msalala Road kata ya Kalangalala,

Mama wa kambo aliyejulikana kwa jina la 
Benitha Augustine,amemchoma mtoto mwenye umri wa miaka minane (8) sehemu mbali mbali za mwili wake na kijiko ambacho alikuwa amekipasha moto kwa madai kuwa alikuwa akimuadhibu .


Akizungumza na waandishi wa habari jirani wa Mama Huyo Bi,Habiba Rajabu alisema Mama huyo amekuwa na tabia ya kumpiga mara kwa mara mtoto huyo bila sababu hali ambayo wao kama majirani wamekuwa wakijiuliza labda kwasababu sio mtoto wake wa kuzaa ndiyo maana amekuwa akimsulubu kwa mateso ya namna hiyo.

“Sisi kama majirani tumeendelea kumshauri kama mtoto amemshinda ni bora akampeleka kwa mama yake kuliko kuendelea kumfanyia vitendo vya ukatili wa namna hiyo amefikia hatua hadi anamchoma na kijiko ambacho amekipasha moto kiukweli inauma sana  ukatili wa namna hii haukubaliki kwenye jamii zetu",alisema Bi Habiba.


Hata hivyo Bi,Benitha Agustine amekiri kufanya kitendo cha kumpiga mwanae na kumchoma kwa kutumia kijiko ambacho amekichemsha kwenye moto na kwamba amekuwa akifanya hivyo kutokana na hasira ambazo zinasababishwa na ugomvi baina yake na mume wake kwani amekuwa akimpiga mara kwa mara  hivyo kuamua kumwadhibu mtoto huyo.

 Katibu wa Mbunge wa viti maalum Chadema Mkoani Geita Shida Mpondi ametoa wito kwa wazazi,walezi na baadhi ya watu wenye tabia za namna hiyo kuachana nazo kwani zinawakosesha haki za msingi watoto na kuwafanya kudumaa kiakili.

Vitendo vya ukatili dhidi ya watoto bado vimeendelea kushamiri mkoani Geita ambapo kuanzia mwezi Januari hadi Juni mwaka Huu jumla ya makosa ya vitendo vya ukatili dhidi ya watoto 199 vimeripotiwa kwenye dawati la jinsia na watoto.


Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye ofisi za polisi Mkoani Geita,Mkuu wa Dawati la Jinsia na Watoto Esnath Magoti ,amefafanua kuwa mchanganuo wa makosa hayo ni kesi za ubakaji,ulawiti ,watoto kutelekezwa ,wengine kutokuwapeleka shule na vitendo vingine vya ukatili dhidi ya watoto.

“Unyanyasaji wa kijinsia bado ni tatizo kubwa sana kwenye mkoa wetu wa Geita ,mara nyingi kesi hizi zinakwama kutokana na jamii kushindwa kuwa na ushirikiano kwa kutoa taarifa wengine wamekuwa wakimalizana wao kwa wao kwenye familia zao hali hii inakwamisha sana jitihada za utetezi wa watoto ambao wanafanyiwa vitendo vya ukatili”,alisema Magoti.

Chanzo - Madukaonline blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post