WAUMINI WAWILI WAFARIKI KWA KUTUMBUKIZWA MTONI NA MTU ALIYEPANDISHA MAJINI WAKATI WAKIBATIZWA


Waumini wawili wa Kanisa Siloam wamekufa maji wakibatizwa katika Mto Ungwasi wilayani Rombo baada ya mmoja wao kupandisha mapepo na kuwatumbukiza majini.


Mkuu wa Wilaya ya Rombo mkoani Kilimanjaro, Agnes Hokororo amethibitisha tukio hilo lililotokea leo, Julai 16 saa sita mchana. Ubatizo huo ulifanyika kwenye kina kirefu cha mto huo.


Amesema wakati ibada ya ubatizo mmoja wa waumini aliyepandisha mapepo alimtumbukiza mmoja wa watu waliokuwa wakisubiri kubatizwa na mchungaji.


Hokororo amesema muumini mmoja alipoona mwenzake ametumbukizwa majini aliamua kumwokoa, ndipo aliyepandisha pepo alipowashikilia wote wawili ndani ya maji na kuwasababishia kifo.


Amesema watu watatu akiwamo mchungaji wa kanisa hilo lililopo katika Kijiji cha Mandechini wanashikiliwa.

Na Fina Lyimo, Mwananchi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527