KAMANDA MPINGA ATEULIWA KUWA KAMANDA WA POLISI MKOA WA MBEYA


IGP Sirro, amefanya mabadiliko katika jeshi la polisi ili kuboresha utendaji wa jeshi hilo kwa kumuhamisha aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Mohamed Mpinga na kuwa Kamanda wa polisi wa mkoa Mbeya


Katika taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi inasema kuwa aliyekuwa Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya (DCP) Dhahiri Kidavashari amehamishiwa Makao Makuu ya upelelezi.


Kufuatia mabadiliko hayo nafasi aliyokuwa nayo Mohamed Mpinga imechukuliwa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Fortunatus Musilimu.


Kwa mujibu wa Barnabas Mwakalukwa (ACP) ambaye ni msemaji wa jeshi la polisi, Makao Makuu ya Jeshi hilo amesema uhamisho huo ni wa kawaida katika kuboresha utendaji wa kazi za Polisi kwa mujibu wa kanuni, taratibu na miongozo ya Jeshi la Polisi.


IGP Saimon Sirro alishauriwa na Rais John Pombe Magufuli kufanya mabadiliko katika jeshi hilo ili kuleta ufanisi na kuboresha utendaji wa jeshi la polisi nchini, jambo ambalo tayari inaonyesha ameanza kulifanyia kazi kwa kufanya mabadiliko kama haya.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post