JAJI MWINGINE AOMBA KUSTAAFU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ameridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Prof. John Eudes Ruhangisa.


Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa Mhe. Rais Magufuli ameridhia maombi ya kustaafu mapema kwa Prof. John Eudes Ruhangisa kuanzia 06 Julai, 2017.


Mhe. Prof. John Eudes Ruhangisa alikuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kanda ya Shinyanga.


Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post