IGP SIRRO: SIKU ZA WAHALIFU KIBITI ZINAHESABIKA


Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro amesema siku zinahesabika kwa wahalifu wote waliojificha mkoani Pwani ambao wamekuwa wakifanya matukio ya uhalifu ikiwa pamoja na kufanya mauaji kwa baadhi ya viongozi na askari polisi nchini.


IGP Sirro amesema hayo jana alipokuwa katika ukumbi wa Police Officer's Mess, Oysterbay Dar es Salaam wakati akikabidhiwa magari manne na kampuni ya kichina ya Great Wall Motors and Haval na kudai kuwa magari hayo yatasaidia kupambana na uhalifu nchini.


"Si kawaida yangu kusema sema ila muda si mrefu nitatoa majibu ya mauaji ya Pwani" alisema Simon Sirro


Pia Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya kichina ya Great Wall Motors and Haval alisema msaada huo wa magari ambao wameutoa kwa jeshi la polisi nchini ni sehemu ya kuunga mkono juhudi kubwa za jeshi hilo katika kupambana na uhalifu nchini.


Mpaka sasa ni zaidi ya watu 30 wamepoteza maisha mkoani Pwani kwa kuuliwa na watu wasiojulikana huku wengine kadhaa wakiwa wamejuruhiwa kwa risasi na watu hao.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post