DC SHINYANGA APIGA MARUFUKU WAGONJWA KUOMBWA FEDHA ZA MAFUTA YA GARI


Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro - Picha kwa hisani ya Malunde1 blog
****
MKUU wa Wilaya ya Shinyanga, Josephine Matiro (pichani) amesema ni marufuku kwa wagonjwa kuombwa fedha za kununulia mafuta ya gari ili wapate huduma ya kusafi rishwa kwenda kupata rufaa hospitali kubwa wakati halmashauri imekwisha tenga bajeti kwa ajili ya mafuta.

Matiro aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati alipokabidhiwa gari la kubebea wagonjwa na Mbunge wa Viti Maalumu, Lucy Mayenga katika Kituo cha Afya cha Kambarage kinachohudumia zaidi ya watu 28,500. Alisema ni marufuku mgonjwa kuombwa fedha kwa ajili ya mafuta kwenye gari ili kupelekwa hospitali kupata rufaa kwani halmashauri imetenga fedha za mafuta na hilo kama la uongo, alimtaka mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo alithibitishe mbele ya wananchi.

Akizungumzia uhaba wa dawa alisema tatizo hilo limekwisha patiwa ufumbuzi mpaka sasa anachokifahamu hakuna tatizo hilo tena kwani serikali imekwishalifanyia kazi na malalamiko madogo madogo yaliyokuwa yakitolewa na wananchi yamekwisha malizwa.

Naye mbunge Mayenga alisema ni bahati kupata gari hilo kwani nchini kuna vituo vingi vya afya, hvyo ni jambo la kushukuru kwani wasingeweza kununua gari hilo kwa haraka lenye thamani ya zaidi ya Sh milioni 290 ikiwa bado kuna changamoto ya ukosefu wa chumba cha upasuaji.






Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga, Laurent Mhembe alisema kituo hicho kilianzishwa mwaka 2010, na kimekuwa na ongezeko la wagonjwa mwaka 2014 baada ya hospitali ya rufaa ya mkoa kupandishwa hadhi na kuwa kituo chenye utegemezi mkubwa.IMEANDIKWA NA KARENY MASASY,- habarileo SHINYANGA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post