MWANAMKE AZIMIA BAADA YA KUVUNJA BANGILI DUKANI

Mwanamke mmoja raia wa China alizirai akiwa kwenye duka la kuuza vito vya thamani baada ya kuvunja kimakosa bangili ghali ya thamani ya dola 44,000.

Mtalii huyo kutoka mkoa wa Jiangxi, alikuwa akijaribu kuvaa bangili hiyo kwenye duka moja lililo mkoa wa Yunnam karibu na mpaka na Myanmar.

Alipoambiwa thamani na bangili hiyo aliivua kwa haraka lakini ikaanguka kimakosa

Hakuna makubaliano yameafikiwa kuhusu vile bangili hiyo itafidiwa.

Wafanyakazi wa duka walijaribu kumtuliza baada ya kisa lakini mara alianza kutokwa na jasho na kisha akazirai.


Alipata nafuu wakati wateja wangine ambao walikuja kumsaidia walipomfinya pua lake.

Wafanyakazi wa duka walimwambia alipe dola 25,000 ili kutatua suala hilo lakini akasema alikuwa na dola 1,500 tu.

Polisi walishindwa kushawishi pande zote kuafikia makubaliano na suala hilo huenda likaelekea mahakamani.

Chama kimoja cha kuuza vito vya thamani kilisema kuwa bangili hiyo ni ya thamani ya dola 26,000.
Via>>BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post