Mtoto (pichani) mkazi wa mtaa wa Mabambasi kata ya Ndembezi katika manispaa ya Shinyanga amefariki dunia leo jioni Jumanne June 27,2017 kwa kutumbukia kwenye ndoo nyumbani kwao.
Mwenyekiti wa mtaa huo David Nkulila amethitisha kutokea kwa tukio hilo.
Kupitia ukurasa wake wa facebook ameandika ujumbe ufuatao
MAJONZI,,,,, Huzuni,,, Hakika kilio.
Nikiwa safarini Serengeti, nimepikea taarifa ya kushitusha na kusikitisha kutokea kwa ajali ya mtoto huyu kutumbukia kwenye ndoo ya maji hadi kusababisha kifo chake. Ee Mungu wa rehema mpokee malaika wako na afurahi na watakatifu wote pema peponi,,,, Hatuna cha kusema bali Ahsante kwani wewe ni mwema daima.
POLENI saana wafiwa na wana mtaa wenzangu Mabambasi kwa msiba huo mzito. Mungu yu pamoja nanyi. ,zaidi nitoe rai tuwe makini na waangalifu saana kwa watoto WETU. Wanahitaji ulinzi kila wakati,,,, tusijisahau,, chonde chonde Nami niko pamoja nanyi kwa maombi,,, POLENI WAPENDWA WANGU