MAMBO MUHIMU KATIKA RIPOTI YA KAMATI YA PILI YA UCHUNGUZI WA MCHANGA WA MADINI,SIKILIZA HAPA



Muhtasari wa Ripoti ya kamati ya Rais Magufuli kama ilivyowasilishwa na Mwenyekiti wake Prof Nehemia Osoro!.

1.Kamati iliandaa mwongozo kazi,kukusanya mikataba,sheria na sera za kodi

2.Kuchambua mfumo mzima wa biashara ya makinikia!.

3,Kutembelea na kupata taarifa kutoka migodini,mamlaka ya bandari,TRA,ofisi ya takwimu,Stamico,Soko la hisa na mitaji,wizara ya nishati na madini!.

4.Kufanya mahojiano na watu kutoka serikalini na watu binafsi!.

5.Kujifunza kutoka nje ya nchi!.

6.Kufanya uchambuzi yakinifu kuhusu biashara ya makinikia tangu mwaka 1998.

7.Kufanya uchunguzi kama kuna uwezekano wa kujenga mtambo wankuchenjua makinikia!.

Matokeo

1.Acacia haijasajiliwa na inafanya biashara isiyo halali

2.Acacia haijawahi wasilisha ripoti yoyote ya kuonesha kuwa wao ni wamiliki wa migodi!.

3.Kamati imebaini Acacia wanafanya biashara kinyume na sheria ya nchi,Acacia hawajulikani kisheria.

4.Kamati imebaini Pangea na Bulyanhulu ndiyo wasafirishaji wa makinikia kutoka Tanzania na hupelekwa China,Japan na Ujerumani yakiwa kwenye makontena ya futi 20 yakiwa tayari yameshauzwa,mauzo hayo hufanya kwa mujibu wa sheria kupitia ofisi ya uhasibu iliyopo Afrika Kusini!.

5.Kamati imebaini kuwa kifungu cha 51 cha sheria ya madini kinamtaka mchimbaji apate kibali kutoka mamlaka,kamati imebaini hakuna utaratibu maalum,kifungu hiki kinataka mwekezaji kutoa taarifa sahihi!.

Kamati imebaini baadhi ya watumishi wa serikali,makampuni ya madini yametenda makosa ya jinai kwa kulisababishi taifa hasara!

Kamati pia imeridhika kuwa baadhi ya watumishi wa serikali na wawekezaji wamelitia aibu taifa kwa kutoa taarifa za uongo!.

Kamati imebaini katika kufanya biashara ya makinikia,makampuni haya yamekuwa yanafanya undanganyifu wa biashara,kutoa taarifa za uongo kuhusu idadi ya makontena na thamani yake!.

6.Makampuni ya makala ya meli yaliwasilisha taarifa za uongo kuhusu biashara ya makinikia!.

Waliruhusu biashara hii ya magendo kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu idadi ya makontena !.

7.Kamati imebaini mauzo ya makinikia hayakufanyika kwa ushindani,makinikia yaliuzwa kwa wafanyabiashara wale wale wenye mahusiano ya wawekezaji!.

Kilichouzwa hakikuwa makinikia hasa,ilikuwa ni madini hasa!.

8.Uchunguzi wa kisayansi kupitia mifumo ya kompyuta ilisababisha gharama za uendeshaji kuonekana kubwa wakati zilikuwa chini na kusabisha wawekezaji kutolipa kodi!.

9.Kamati imebaini kuwa Bulyanhulu na Pangea hawakuonesha faida wanayopata kwenye biashara!.

10.Kamati imebaini faida iliyooneshwa imekuwa ikirudishwa kwenye makampuni kama mikopo kwa kutumia riba!.

11.Kamati imebaini makinikia yaliyosafirishwa tangu mwaka 1998 kuwa makontena 44,227-61,320 sawa na shilingi Trilioni 108 za kitanzania kwa kiwango cha chini huku kiwango cha juu ikiwa ni Trilioni 180!.

Thamani ya silver toka mwaka 1998 ni shilingi bilioni 366.66,Copper ni Trilioni 2.86,surphure ni Trilioni Bilioni 277.393,Chuma ni shilingi Bilioni 368.2.,Zinc bilioni 8.42,Nicol trilion 13.22,uradium trilioni 17.19,metal Trilion 1.9.

Kifupi tangu mwaka 1998,nchi imepoteza kiasi cha Shilingi Trilion 132.56 kwa kiwango cha chini na Trilioni 200.9 kwa kiwango cha juu!.

Upande wa Makinikia serikalinimepoteza Trilion 149-253.8 
Silver ni Trilion 5,Copper trilion 3.9,Surpher,Bilioni 411,

Thamani ya madini yote kati ya mwaka 1998 hadi sasa ni shilingi Trilion 188.59-380.99

Kiwango cha mapato kilichopotea,ni Trilion 55(kodi ya mapato,Bilioni 94(Withholding tax),Mrahaba(Trilion 11) Gharama za meli Trilion (1.6)

Pesa zilizopotea zingeweza hudumia bajeti ya miaka mitatu ama kujenga reli ya standard kutoka Dsm mpaka Mwanza!

KUHUSU Makinikia

1.Kamati imebaini serikali siyo sehemu ya mkataba wa biashara ya makinikia!.

2.Mikataba haina sehemu ya masharti ya kuwataka wawekezaji kutoa taarifa za uuzwaji wa makinikia,serikali imekuwa haipati taarifa halisi

Kuhusu Mikataba ya madini

1.Kamati imebaini serikali iliingia mkataba na mwekezaji wa mgodi wa Kahama,lakini hakuna sehemu inayoonesha serikali kupata pesa za kutosha,serikali ilifikia hatua ya kupunguza hisa zake kutoka 15 mpaka 5 na kujikuta ikipata dola laki moja tu,mabadiliko haya yalifanywa na Dr Kigoda!

2.Mkataba kati ya Pangea ulisainia na Daniel Yona na Karamagi na serikami haijawahi pata chochote kutokana na kukosa hisa!.

3.Mkataba kati ya serikali ya North Mara ukiosainiwa na Daniel Yona,serikali haina hisa hata moja,mwaka 2007,serikali ilijifutia hisa zote!.

4. Mkataba kati ya GGM na serikali ulisainiwana Daniel Yona,hapa napo serikali haina hisa hata moja!.

5.Kamati imebaini kuwa kumekuwa na uongezwaji wa mikataba inayofanywa na serikali,waliohusika ni Willium Ngereja,Prof Muhongo,wanasheria wa serikali!.

6.Kamati imebaini kuwa sheria haizuii serikali kubadili sheria na sera!

7.Kamati imebaini mikataba inaweza kurekebishwa kwa maslahi ya taifa/nchi!.

8.Kuhusu misamaha ya kodi,kamati imebaini misamaha inayosababisha hasara!.

9.Kamati imebaini kuwa makampuni haya yamekuwa hayaweki fedha kwenye mabenki ndani!.

10.Kamati imebaini makampuni haya kuajiri wazawa kwenye maeneo yenye wataalam,kamati imebaini kuwa hakuna utaratibu madhubuti uliowekwa na serikali kuhakikisha kigezo hiki kinatekelezwa!.

11.Kamati imebaini kuwa makampuni yamekuwa yakichangia kiasi kidogo kwenye shughuli za maendeleo ya jamii!.

12.Kamati imeona kuwa waziri amekuwa na madaraka makubwa,kamati imebaini kuwa bunge lipewe nguvu na siyo waziri pekee!.

13.Kamati imependeleza sheria ya madini ifanyiwe mapitio!.

14.Kamati imebaini kuwa nchini inaweza kujenga mtambo wa kuchenjua makinikia hapa nchini!.

14.Kamati imebaini kuwa nchi haina taasisi zinazosimamia biashara ya madini,tangu serikali iivunje Nasaco makampuni ya usafirishaji yamekuwa yakifanya kazinya Nasaco(yanajikagua yenyewe).

MAPENDEKEZO YA KAMATI

1.Hatua za kisheria zichukuliwe dhidi ya Acacia

2.Serikali idai kodi na makampuni yote yaliyokwepa kodi!.

3.Usafirishaji wa makinikia usitishwe mpaka kodi ilipwe

4,Mtambo wa kuchenjua makinikia ujengwe!.

5.Waliohusika wote katika kuingia mikataba wachukuliwe hatua za kisheria!.

6.Utaratibu wa malipo ya mrahaba ufutwe!.

7.Serikali ifanye uchunguzi kuhusu mwenendo wa watumishi wa mabaraza ya kodi!.

8.BOT ifuatilie malipo ya mrahaba

9.Serikali ianzishe utaratibu wa ulinzi kwenye migodi

10.Adhabu za waliokiuka sheria ziongezwe!.

11.Mikataba yote ya madini ipitiwe upya!.

12.Sheria iweke kiwango maaluma cha hisa!.

13.Serikali iunde chombo cha kusimamia ustawishaji wa biashara!.

14.Sheria iseme madini ni malinya watanzania chini ya udhamini wa rais

15. Mikataba yote iwe wazi

16.Madaraka ya waziri na kamishna yapunguzwe!.

17.Suala la ajira na mafunzo kwa wazawa izingatiwe!.

18.Fedha za mauzo ya madini ziwekwe kwenye mabenki!.

19.Serikali ifute ama izifanyie marekebisho kwenye sheria za kodi na madini!.

20.Serikali itoe mafunzo ya mara kwa mara kwa watumishi wake!.

21.Serikali iwe inafanya ukaguzi wa mara kwa mara!
 SIKILIZA HAPA 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post