MAHAKAMA YAAMURU KABURI LA TAJIRI WA UGANDA IVAN ALIYEZIKWA NA MAMILIONI YA FEDHA LIFUKULIWE | MALUNDE 1 BLOG

Friday, June 2, 2017

MAHAKAMA YAAMURU KABURI LA TAJIRI WA UGANDA IVAN ALIYEZIKWA NA MAMILIONI YA FEDHA LIFUKULIWE

  Malunde       Friday, June 2, 2017
Wanasheria nchini Uganda wameamua kuifikisha familia ya Ivan Mahakamani kwa makosa ya kuzika pesa halali za Jamhuri ya Uganda katika kaburi la ndugu yao Ivan. Kwa nchi yoyote kitendo hicho hakikubaliki kwani pesa hizo zingeweza kutumika katika shughuli zingine na kukuza uchumi wa nchi.

Kitendo hicho kinakuja baada ya marafiki wa Ivan kumwaga mamilioni ya pesa ndani ya kaburi la Ivan kama njia ya kumuaga rafiki yao aliyekuwa maarufu kwa matumizi makubwa ya pesa.

Wanasheria wakiongozwa na Tugume Gideon wa Human Rights Defenders Association Uganda wamesema hawakufurahishwa na kitendo cha RICH GANG cha kuzika mamilioni ya pesa ndani ya kaburi, na kwa vile ni kinyume cha sheria,

wameamua kwenda mahakamani kuomba kaburi la Ivan lifukuliwe, pesa zitolewe zikafanye shughuli nyingine na waliohusika washitakiwe kwa kuharibu kwa makusudi alama ya taifa.
Advertisement
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post