Msanii wa muziki wa bongo kutoka Tanzania Diamond Platinums sasa amepanua biashara yake katika harakati za kuwafurahisha mashabiki na wateja wake.
Msanii huyo alizindua bidhaa ambayo sasa iko madukani nchini Kenya.
Huku wasanii wengi wakitumia muda wao mwingi kuuza tisheti, Diamond alianzisha manukato ya Chibu ambayo ni bidhaa ya kipekee.
Msanii huyo baadaye alifanya kile ambacho wengi hawakutarajia kwa kuzindua njugu karanga siku ambayo alimkaribisha Rayvanny nchini Tanzania.
Hivi ndivyo alivyoandika katika chapisho lake la akaunti yake ya facebook siku ya Alhamisi:
USISEME KARANGA SEMA DIAMOND KARANGA!!!!...Habari njema kwa Vijana wenzangu wote, sasa unaweza kujipatia Mtonyo wa ChapChap kupitia @diamondkaranga ambapo utaweza kununua kwa bei ya jumla ya shilingi elfu ishirini (20,000) kwa boksi moja lenye pakiti Mia moja (100) ndani ambazo ukiuza unapata faida ya elfu kumi fanya mawasiliano sasa na mawakala walio karibu yako.