DC APIGA MARUFUKU UINGIZAJI NA UCHINJAJI WA NGURUME DODOMA



MKUU wa wilaya ya Dodoma Christina Mndeme (pichani) amepiga marufuku uingizaji na uchinjaji wa nguruwe,kutokana na kuingia kwa mlipuko wa homa ya nguruwe ambao mpaka sasa zaidi ya 200 tayari wameshakufa.


Mkuu huyo wa wilaya pia amewataka wakazi wa manispaa ya Dodoma kutokula mizoga ya nyama hiyo,ili kuepukana na maambukizi ya homa ya nyama ya nguruwe ambayo kwa asilimia mia moja inaua kwa binadamu wanaotumia badala yake wahakikishe wanakula iliyopimwa na wataalamu wa afya.


Mndeme ametoa onyo hilo wakati akizungumza na madiwani na watendaji wa manispaa ya Dodoma na kuwataka kutoa elimu kwa usahihi kwa wananchi wao juu ya madhara ya mlipuko huo uliojitokeza wa homa ya nguruewe.

Alisema kutokana na kujitokeza kwa ugonjwa huo mpaka sasa kata zinazoongoza kwa vifo vya nguruwe hao zipo mbili nazo ni pamoja na Ipagala na Miyuji ambapo zaidi ya 200 wameshakufa.tayari.

Akizungumza na madiwani hao pamoja na watendaji amewataka kuhakikisha wanatoa elimu ya kutosha kwa wananchi ukiwa na pamoja kufanya doria kuwakamata wale wote watakaobainika kukaidi amri hiyo.

“Ninawaagiza nyinyi madiwani pamoja na watendaji hakikisheni mtoa elimu iliyo sahihi iliyo wazi bila kificho,ukizingatia kuwa ugonjwa huo homa ya nguruwe unaua tena kwa aslimia mia moja,hivyo ni marufuku kuingiza ndani ya wilaya hii na wala kuchinja pasipo ruhusiwa na wataalamu wa afya”alisema.


Alisema pamoja na ufugaji wa nguruwe ni sehemu ya kujiingizia kipato kwa kipindi hiki ambacho mlipuko huo umejitokeza wa homa hiyo,hakuna sababu ya kupuuza bali wanatakiwa kujiepusha ulaji holela wa nyama kwenye maeneo yanayouzwa.

Hata hivyo amewataka wafugaji wa nguruwe pia kujiepusha na uchukuaji wa vyakula vinavyobaki kwenye mahoteli na sokoni kwa kuwa vinasadikika kuwa na vimelea inayochangia kuwepo kwa homa hiyo kwa wanyama hao.
Na Josephine Charles-Malunde1 blog Dodoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post