NAPE NNAUYE AWAPONDA WABUNGE WA CCM WANAOSIFIA SERIKALI KWA KILA KITU

Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye amefunguka na kusema wabunge wa Chama Cha Mapinduzi ambao wanaishauri na kuikosoa serikali ni watu ambao wana mapenzi mema na Rais na serikali yake kuliko wanao sifia kila kitu.

Nape Nnauye amedai wabunge ambao kazi yao ni kusifia kila kitu hata kama kuna mapungufu hao hawana mapenzi ya kweli kwa Rais Magufuli na serikali kiujumla na kudai yeye anaitumia nafasi yake vizuri kutoa ushauri kwa serikali kupitia bunge sababu ndiyo njia sahihi aliyonayo kwa sasa.

"Kimsingi kazi kubwa ya Mbunge hasa wabunge wa CCM ni kuishauri serikali yake sisi tunaoshauri tunampenda zaidi Rais na tunaipenda zaidi serikali ifanye vizuri kuliko wale ambao watakuja na kusifu na kupongeza kwa kila kitu, hata pale wanaona kabisa hapa tungeweza kushauri na mambo yakarekebishika" alisema Nape Nnauye

Mbali na hilo Nape Nnauye amedai kuwa watu ambao wanashangaa yeye kuishauri serikali sasa kupitia bunge anasema hawafahamu pia alipokuwa kwenye Baraza la Mawaziri, alikuwa akifanya hivyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527