Wanafunzi 29 , walimu 2 na dereva wa gari la shule ya msingi iitwayo Lucky Vicent ya Arusha wamefariki dunia leo saa 3 asubuhi baada ya gari walilokuwa wakisafiria kupata ajali katika eneo Rhotia Marera, Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha.
Wanafunzi na walimu hao walikuwa wakitoka shuleni kwao kwenda shule ya msingi iitwayo Tumaini kwa ajili ya kufanya mtihani wa ujirani mwema na walipofika katika eneo la Rhotia Marera basi walilopanda liliacha njia na kisha kutumbukia korongoni ambako limesababisha vifo hivyo na majeruhi watatu.
Majina ya marehemu.
Majina ya marehemu yaliyotajwa hadi sasa kutokana na ajali hiyo ni Mteage Amos, Justine Alex, Irene Kishari, Praise Ronald, Shadrack Biketh, Junior Mwashuya, Aisha Saidi, Heri Rashid, Gema Gerald, Rebecca Daudi, Hagai Lucas, Sada Ally, Lucy Ndemna, Mussa Kasim na Neema Martin. Wengine ni Witness Mosses, Rukia Khalfani, Naomi Hosea, Hevenight Hosea, Eliapenda Eliudi, Arnold Alex, Marion Mrema, Rehema Msuya, Sabrina Said, Prisca Charles, Grayson Robson Massawe, Lara Tarimo na Neema Eliwahi.
Wote walikuwa wanafunzi wa darasa la saba ambao walikuwa wafanye Mtihani wa Taifa wa Shule Msingi 2017 . Shule hiyo pia iliongoza mitihani ya taifa mwaka jana. Shule ya Awali na Msingi ya Lucky Vincent ambayo wanafunzi wake wameteketea katika ajali hiyo jana asubuhi waliongoza mwaka jana katika Mtihani wa Taifa Kimkoa.
Shule hiyo iliyopo eneo la Field Force, Kwa-Mrombo katika kata ya Olasiti, mjini Arusha ilikuwa shule ya 20 bora kati ya shule 8,109 nchini na katika Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba mwaka jana ilikuwa na wahitimu 101 na wanafunzi wote waliofanya mtihani walipata Daraja A katika somo la Kiingereza.
Shule ya Msingi Lucky Vincent ilikuwa shule namba moja mkoani Arusha na kuzishinda shule nyingine za msingi 331 katika wilaya saba za mkoa huo. Wakati wanafunzi wote wa Lucky Vincent walipata ‘A’ kiingereza, wanafunzi 92 walipata ‘A’ kwenye somo la sayansi , 81 walipata ‘A’ ya hesabu na 63 walipata ‘A’ Kiswahili (63), ikionesha walikuwa wazuri katika masomo ambayo wengine wanayaona magumu sana.
Hapa chini ni majina ya wanafunzi waliofariki katika ajali hiyo