BINTI WA MIAKA 35 AJITOKEZA KUWANIA URAIS NCHINI RWANDA

Mwanadada Diane Rwigara, ametangaza azma yake ya kuwania Urais nchini Nchini Rwanda katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti mwaka huu.


Huyu ni Binti wa mfanyabiashara maarufu wa Kinyarwanda Assinapol Rwigara aliyefariki miaka 2 iliyopita katika mazingira ya kutatanisha .


Bi Diane mwenye umri wa miaka 35 amesema, anataka kukomesha uonevu na kuleta haki na uhuru wa watu kujieleza nchini Rwanda.


Amesema, kuna suala la usalama mdogo ambapo baadhi ya watu hutoweka na wengine kuuwawa katika mazingira ya kutatanisha, na kwamba huwezi kusema uko katika nchi yenye amani na usalama wakati watu wanauawa huku wengine wakikimbia nchi.


Huyu ni Mnyarwanda wa tatu kutangaza rasmi nia ya kutaka kugombea urais nchini Rwanda wengine wakiwa ni Bwana Mpayimana Philippe aliyetangaza kuwa mgombea binafsi na Franck Habineza kutoka chama cha Green.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post