Picha: VIONGOZI WA SERIKALI WASHUHUDIA HALI MBAYA YA MTO RUAHA MKUU...DKT. KIJAZI ATOA WITO KUUNUSURU


Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan na viongozi mbali mbali wakitazama mto Ruaha mkuu unavyokauka leo kutoka kushoto Mkurugenzi wa TANAPA Dkt Allan Kijazi, waziri wa ardhi, nyumba na makazi William Lukuvi na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza 
Waziri Lukuvi akimwonyesha makamu wa rais kiboko 
Mkurugenzi mkuu wa Tanapa Dkt Allan Kijazi akionyesha jinsi mto Ruaha mkuu unavyo kauka mbele ya makamu wa Rais 
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan Kushoto na mkuu wa mkoa wa Iringa Amina Masenza na waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Wiliam Lukuvi leo wakati wa kutembelea eneo la mradi wa ikolojia mto Ruaha mkuu leo kushoto mwenye miwani ni waziri wa mazingira na muungano January Makamba 
Mwanahabari Tukuswiga Mwaisumbe ambae katibu wa IPC akitazama Ikolojia ya mto Ruaha mkuu 
Katibu tawala wa mkoa wa Iringa Ayubu Wamoja akitazama mradi wa hifadhi ya Ikolojia mto Ruaha mkuu leo 
Waziri wa mazingira na Muungano January Makamba akitazama mto Ruaha mkuu leo 
Mwanahabari Adam Mzee kutoka ofisi ya makamu wa Rais kulia akiwa na mzee wa matukiodaima leo 

Picha zote kwa hisani ya Matukodaimablog

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ameuahidi uongozi wa Hifadhi ya Taifa ya Ruaha na wa Mkoa wa Iringa kuwa Serikali italifanyia kazi tatizo la ubovu wa barabara kutoka Iringa mjini Hadi katika hifadhi hiyo ili kuongeza idadi ya watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo katika mkutano wake na Viongozi wa Hifadhi hiyo na wa mkoa wa Iringa baada ya kufanya ziara fupi katika hifadhi hiyo pamoja na kujionea utiririshaji hafifu wa maji katika Mto Ruaha uliosababishwa na shughuli za kibinadamu hasa kilimo.

Makamu wa Rais amesema serikali itahakikisha barabara hiyo inajengwa kwa awamu kwa kiwango cha lami kama hatua ya kuongeza maradufu idadi ya watalii katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha ambapo kutokana na ubovu wa barabara kuelekea hifadhi hapo idadi ya watalii wanaotembelea hifadhi hiyo imeendelea kupungua kila uchao.

Kuhusu vitendo vya ujangili hifadhi hapo, Makamu wa Rais ameuagiza uongozi wa hifadhi hiyo kushirikiana na wananchi wanaozunguka hifadhi hiyo ili kuwabaini majangili na kuwachukulia hatua ili kukomesha vitendo hivyo.

Amesema idadi kubwa ya majangili wanatoka miongoni mwa jamii zinazozunguka Hifadhi ya Taifa ya Ruaha hivyo wananchi wakishirikishwa kikamilifu katika kutoka taarifa za siri majangili wengi watakamatwa na kuwajibishwa.

Awali akitoa taarifa kwa Makamu wa Rais, Kuhusu utendaji kazi wa Hifadhi hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) ALLAN KIJAZI aliiomba serikali isaidie kulinusuru bonde la Usangu ili liweze kurejesha mtitiriko wa maji kwa ajili ya matumizi ya hifadhi hiyo na kumaliza mgogoro wa mpaka kati ya hifadhi na wananchi ambao umedumu kwa muda mrefu bila suluhu kupatikana.

 Amesema mpaka sasa TANAPA imeshatumia zaidi ya shilingi bilioni Saba kwa ajili ya kulipa fidia wananchi na gharama nyingine ili kunusuru bonde hilo lakini bado kuna changamoto ambazo zinaathiri usimamizi wa eneo hilo na zinahitaji maamuzi ya serikali.

Mkurugenzi huyo Mkuu wa TANAPA pia amepongeza msukumo wa dhati wa serikali ya awamu ya Tano katika kusimamia hifadhi ya mazingira na maliasili kwani jitihada hizo zitasaidia kuboresha mazingira na viumbe hai kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post