Picha: KONGAMANO LA WADAU WA WAKALA WA USALAMA NA AFYA MAHALI PA KAZI - OSHA LAFANYIKA MOSHI ,MGODI WA BUZWAGI WASHIRIKIKatika kuadhimisha wiki ya usalama na afya kazini mwaka 2017, Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (Occupational Safety and Health Authority - OSHA) imefanya kongamano kwa kuwakutanisha kwa mara ya kwanza wadau wa OSHA nchini kwa lengo la kubadilishana uzoefu katika masuala ya afya na usalama mahali pa kazi.

Kongamano hilo limefanyika leo Alhamis Aprili 27,2017 katika ukumbi wa Chuo Cha Ufundi Stadi - VETA Moshi mkoani Kilimanjaro.

Miongoni mwa washiriki wa kongamano hilo ni kampuni ya uchimbaji madini ya Acacia inayomiliki migodi ya dhahabu ya Buzwagi,Bulyanhulu na North Mara ambao wamefuzu mafunzo mbalimbali ya usalama kazini yaliyotolewa na OSHA.

Akizungumza wakati wa kufungua kongamano hilo, Kaimu Mtendaji Mkuu wa OSHA Hadija Mwenda alisema wanafarijika kuona jinsi makampuni ya uchimbaji madini nchini yalivyohamasika katika kuimarisha masuala ya afya na usalama kwenye maeneo ya kazi.

Mwenda alisema bado jamii inaamini kuwa masuala ya usalama mahali pa kazi ni ya watu wachache hivyo kuwataka wadau wengine kuiga mfano wa makampuni ya uchimbaji madini ambao mbali na kuimarisha hali ya afya na usalama kazini pia wamejitokeza kwa wingi kuonesha kazi zao katika wiki ya afya na usalama kazini mwaka 2017.

“Watu wanadhani suala la usalama ni la wachache ndiyo maana hata washiriki wengi wa maonesho ya wiki ya usalama mahali pa kazi ni watu wa migodi,naomba jamii ielewe kuwa suala la afya na usalama ni la watu wote kwani tukizingatia usalama kazini tunajiepusha na magonjwa na vifo”,alieleza Mwenda.

“Ili kuonesha OSHA tunajali na kumuunga mkono rais John Pombe Magufuli katika suala la uchumi wa viwanda kwa mara ya kwanza tumekutana katika mkutano wa pamoja na wadau wetu ili tupate mrejesho wa nini taasisi zinafanya katika kuimarisha afya na usalama kazini kwa lengola kuboresha zaidi”,aliongeza Mwenda.

Akiwasilisha mada kuhusu namna mgodi wa Buzwagi unavyohakikisha kuna usalama mgodini,Afisa Usalama na afya wa mgodi huo Mustapha Mlewa alisema mgodi wao umeweka mstari wa mbele suala la afya na usalama kazini.

Alisema mgodi huo unatekeleza mradi wa Tunajali kwa kuwafundisha wafanyakazi wao namna ya kutambua vihatarishi, kujilinda wawapo mgodini lakini pia namna ya kutumia vifaa mbalimbali vya uokozi kwenye maeneo yao ya kazi.

Nimekuwekea hapa picha za matukio wakati wa Kongamano hilo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Hadija Mwenda akifungua kongamano la wadau wa Osha katika ukumbi wa VETA Mjini Moshi
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Hadija Mwenda akielezea umuhimu wa taasisi mbalimbali za serikali na binafsi kuboresha mfumo wa afya na usalama mahali pa kazi
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Hadija Mwenda akizungumza ukumbini
Maafisa kutoka mgodi wa dhahabu Buzwagi wakisikiliza kwa makini hotuba ya Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Hadija Mwenda.Katikati ni Afisa Usalama na afya mgodi wa Buzwagi Deogratius Nyantabano akifuatiwa na afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa (kulia)
Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Hadija Mwenda akizungumza ukumbini
Maafisa kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) wakiwa ukumbini wakifuatilia yaliyokuwa yanajiri
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akitoa mada kuhusu namna mgodi wa Buzwagi unavyozingatia masuala ya afya na usalama mgodini
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akitoa mada kwenye kongamano la wadau wa OSHA katika ukumbi wa VETA Mjini Moshi
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akitoa mada ukumbini 
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akielezea malengo ya mgodi huo kupitia mpango wa Tunajali / WE CARE
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akielezea namna wanavyojali wafanyakazi wao wawapo mgodini
Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Joshua Matiko akitoa mada kwenye kongamano hilo
Mkurugenzi wa Mafunzo na Utafiti kutoka Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) Joshua Matiko 
Afisa usalama na afya mgodi wa Buzwagi Mustapha Mlewa akichangia hoja wakati wa kongamano hilo.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post