MRADI WA ECOPRC WAWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WA HABARI JUU YA USIMAMIZI SHIRIKISHI WA MISITU NA MABADILIKO YA TABIA NCHI, MJINI MOROGORO


Mratibu wa Mradi wa kuwajengea uwezo jamii kupitia mafunzo ya usimamizi shirikishi wa misitu, Mkuhumi na mabadiliko ya Tabia Nchi (ECOPRC), Bw. Elinasi Monga akifundisha somo la mabadiliko ya tabia nchi ambalo aliweza kukazia suala la waandishi wa habari kujua visababishi na viashiria ambavyo ni vyema kujua na kuweza kuvifanyia kazi kwa ufasaha zaidi. Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro. Picha zote na Cathbert Angelo Kajuna wa Kajunason Blog.


Katika mafunzo hayo Mratibu wa Mradi huo alisema kuwa wakulima wadogo wadogo ndiyo wanaathika zaidi na mabadiliko ya tabia nchi kwa kuwa wamekuwa hawana uelewa mzuri katika masuala ya mabadiliko ya tabia nchi.

Aliongeza jambo lingine linalorudisha nyuma ni serikali za mitaa kukosa mipango mikakati ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Aidha alisisitiza uongozi mbovu katika sekta ya misitu huchangia uharibifu wa misitu kwa kiasi kikubwa.

`
Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Elinasi Monga akisisitiza jambo.
Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Richard Giliba akifundisha somo juu ya kiwango vya athari ya mabadiliko ya tabia nchi, Nyenzo shirikishi pamoja na umuhimu wa misitu ya jamii ambavyo ni muhimu kwa waandishi wa habari kujua na kuvifanyia kazi. Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro.
Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Richard Giliba akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari waliohudhiria mafunzo hayo.
Kikundi cha tatu kikijadiliana.
Kikundi cha pili kikijadiliana.
Kikundi cha kwanza wakijadiliana.

Waandishi wa habari wakifuatilia mafunzo.
Mratibu wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Daniel Lucas akifundisha somo juu ya kuimarishwa Utawala Bora katika Usimamizi Shirikishi wa Misitu ambavyo ni muhimu kwa waandishi wa habari kujua na kuvifanyia kazi. Mafunzo hayo yaliyoanza Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro.
Meneja wa Mradi wa ECOPRC), Bw. Almas Kashinde (kulia) akifunga mafunzo ya waandishi wa habari yaliyofanyika Aprili 3 - 7, 2017 mjini Morogoro.

Alisema kuwa nia ya nia ya mradi wa ECOPRC ni kuziwezesha jamii ziishizo vijijini na wadau wengine kupitia mchakato mahsusi wa kuwajengea uwezo ili kuboresha Usimamizi Shirikishi wa Misitu na kuwa na uboreshaji wa njia za maisha katika jamii. lengo la mafunzo haya ni kuhamasisha serikali katika Usimamaizi Shirikishi wa Misitu ili kuwa na faida za kijamii, kiuchumi na kimazingira kwa jamii zinazojihusisha na Usimamizi Shirikishi wa Misitu. Kushoto ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. 
Meneja wa Mradi wa kuwajengea uwezo jamii kupitia mafunzo ya usimamizi shirikishi wa misitu, Mkuhumi na mabadiliko ya Tabia Nchi (ECOPRC), Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Mussa Twangilo (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. 
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, James Lyatuu (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. 
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Henry Mwakifuna (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. 
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Beatrice Philemon (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. 
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Safia Maftah (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. 
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Saada Mbarouk (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. 
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa Blogger na mwandishi wa habari, Cathbert Angelo Kajuna (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. 
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Josephine Mallango (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. 
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Agrey Evarist (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. 
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Kalokola Aporinary (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba. 
Meneja wa Mradi wa ECOPRC, Bw. Almas Kashinde (kulia) akitoa cheti kwa mwandishi wa habari, Prosper Kaijage (kushoto) mara baada ya kumaliza mafunzo yaliyoanza Aprili 3-7, 2017 mjini Morogoro. Katikati ni Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Richard Giliba.
Waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo ya Mradi wa kuwajengea uwezo jamii kupitia mafunzo ya usimamizi shirikishi wa misitu, Mkuhumi na mabadiliko ya Tabia Nchi (ECOPRC) mjini Morogoro wakiwa katika picha ya pamoja na wawezeshaji wao.

Kuhusu Mradi wa ECOPRC

Mnamo tarehe 25 Oktoba 2012, Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Ufalme wa Norway zilikubaliana kuingia katika mkataba wa utekelezaji wa Mradi wa kuwajengea uwezo Wananchi kupitia Mafunzo ya Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USM), Mpango wa Kupunguza Uzalishaji wa Hewa Ukaa Kutokana na Ukataji na Uharibifu wa Misitu (MKUHUMI) na Mabadiliko ya Tabianchi (“Empowering Communities through Training on Participatory Forest Management, REDD+ and Climate Change Initiatives – ECOPRC”). 

Lengo kuu la mradi huu ni kujenga uwezo wa vikundi mbalimbali vya kijamii ili viweze kusimamia misitu kwa uendelevu na kwa faida; lengo mahususi ni kuongeza tija katika usimamizi endelevu wa rasilimali za misitu kwa namna ambayo inaleta faida kijamii, kiuchumi, kimazingira na kiutawala bora kwa jamii zinazojihusisha na shughuli za Usimamizi Shirikishi wa Misitu, MKUHUMI na Mabadiliko ya Tabianchi.

Mradi huu ni wa miaka mitano, unaotekelezwa na washirika wanne ambao ni Chuo cha Misitu Olmotonyi (Mshirika Kiongozi), Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA); Kituo cha Misitu na Watu (RECOFTC) cha Bangkok-Thailand na FORCONSULT, kitengo cha ushauri elekezi cha Kitivo cha Misitu na Hifadhi ya Mazingira Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine. Shughuli za Mradi zinatekelezwa katika malengo mahususi sita: 

1. Programu ya kujenga uwezo wa Taifa katika USM/MKUHUMI umeandaliwa na kurasimishwa kupitia mafunzo yatokanayo na uzoefu na uwezo wa kusharadiana na mazingira halisi.

2. Ufanisi na Uwajibikaji wa Halmashauri za Wilaya na Watumishi wake Unaongezeka Kwa Kutoa huduma bora kwa wananchi na wadau katika nyanja za USM, MKUHUMI na Mabadiliko ya Tabianchi.

3. Kuboresha Maarifa na Uelewa wa Viongozi wa Vijiji Katika usimamizi endelevu wa shughuli za USM, MKUHUMI Mabadiliko ya Tabianchi. 

4. Kutoa Fursa kwa Watendaji, Watekelezaji na Watoa Maamuzi ili Waweze Kupitia, kufanya Mageuzi na Kutambua Mazingira Wezeshi kwa Sera za USM, MKUHUMI na Mabadiliko ya Tabianchi.

5. Miundombinu ya Chuo cha Misitu inaboreshwa ili kuongeza ufanisi katika kutoa Mafunzo bora

6. Usimamizi na Uendeshaji wa Mradi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post