MBUNGE WA NZEGA HUSSEIN BASHE ADAI KUTEKWA...AWATAKA WABUNGE WAACHE UNAFIKI

Mbunge wa Nzega Mjini(CCM) Hussein Bashe amewataka wabunge wa CCM kuacha unafiki kuhusu kuwateka watu na kwamba yeye ni mmoja wa watu waliokamatwa na usalama wa taifa wakati wa mkutano Mkuu wa CCM.


"CCM acheni unafiki mimi nimeshakamatwa na watu wa usalama mnasema hawakamati, kwa hili nipo tayari mniondoe kwenye chama". Amesema Bashe


Bashe alikuja juu baada Waziri wa Tamisemi, George Simbachawene kumtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe kuthibitisha kuwa matukio ya ukamataji yanafanywa na usalama wa Taifa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post