News Alert : POLISI NANE WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI PWANI...RAIS MAGUFULI AWALILIA

Askari polisi nane waliokuwa katika doria kijiji cha Jaribu mpakani mwa wilaya za Rufiji na Kibiti mkoani Pwani nchini Tanzania wanadaiwa kuuawa kwa kupigwa risasi usiku wa Aprili 13,2017.Mkuu wa jeshi la polisi Tanzania IGP Ernest Mangu amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa taarifa zaidi zitatolewa na kamanda wa polisi mkoa wa Pwani.

Taarifa zinasema kuwa polisi hao walikuwa kwenye gari wakirejea kituoni kutoka kwenye doria na walishambuliwa na watu waliotokea msituni.

Imeelezwa kuwa majambazi hao waliwavamia ghafla polisi hao waliokuwa kwenye gari na kuwapiga risasi na kuwaua wote palepale eneo la tukio, kisha kutokomea kusikojulikana na kwamba silaha zote walizokuwa nazo (SMG) zilichukuliwa na watu hao.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post