Mbunge wa Chemba Juma Nkamia leo alipata nafasi ya kusimama Bungeni Dodoma katika kuchangia maoni kuhusu mapitio ya mapato na matumizi ya fedha za ofisi ya Waziri mkuu na ofisi ya bunge kwa mwaka wa fedha 2017/2018.
Katika vitu alivyoongelea Nkamia ni kitendo cha Waziri wa Habari, utamaduni, sanaa na michezo Dr. Harrison Mwakyembe kwenda katika mkutano wa msanii Roma mkatoliki alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Dar es salaam jana.
Amesema: Jana nilipata nafasi ya kuangalia Press Conference ya Roma. Najiuliza, Waziri wa habari alienda kufanya nini? Akiambiwa ndo alimteka Roma atakataa?
"Mtu alitekwa, serikali ndiyo inamwandalia press conference na kuisimamia? hivi kesho mkiambiwa ndiyo mlihusika kumteka mtakataa? Najua ukweli unauma, lakini lazima tuseme.
"Serikali wakati mwingine mnaingia kwenye mitego wenyewe na mnamgombanisha Rais na wananchi.
"Nimesema ukweli, wengine wataanza kuwaza labda ni kwa sababu nilikosa uwaziri.....No, lazima tuseme ukweli."
SIKILIZA HAPA CHINI