HAYA HAPA MAJINA YA WABUNGE WA TANZANIA WATAKAOWAKILISHA KATIKA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Jana Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipiga kura kuchagua wabunge watakaoiwakilisha nchi katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EALA) kwa kipindi cha miaka mitano.

Baada ya mvutano wa muda mrefu kuhusu uchaguzi huo, ulifanyika na Spika wa Bunge, Job Ndugai kutangaza orodha ya washindi waliochaguliwa kuiwakilisha nchi.

Tanzania inatakiwa kutoa wabunge 9 kwenda EALA, lakini matokeo ya jana yalitangaza washindi saba tu baada ya wagombea wawili kupigiwa kura nyingi za hapana, na hivyo kuonekana kuwa wabunge hawakuwataka.

Kati ya wabunge 7 waliotangazwa, 6 ni wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na mmoja na wa Chama cha Wananchi (CUF).

Wagombea wa CHADEMA, Lawrence Masha na Ezekiah Wenje walipingwa kwa kupigiwa kura nyingi za hapana.
  1.      Fancy Nkuhi (CCM)
  2.     Happiness Legiko (CCM)
  3.     Maryam Ussi Yahya (CCM)
  4.     Dkt Abdullah Makame (CCM)
  5.     Dkt Ngwaru Maghembe (CCM)
  6.     Alhaj Adam Kimbisa (CCM)
  7.     Habib Mnyaa (CUF)
Baada ya matokeo hayo kutangazwa, Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe akizungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge alisema kuwa, hawayakubali matokeo hayo na kuwa watakwenda mahakamani.

Mbowe pia amemtuhumu Rais Dkt Magufuli na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuhusika katika mchakato wa kuwakataa wagombea wa CHADEMA na kusema kuwa, wao hawatakubaliana na hilo kwa sababu Spika wa Bunge amekiuka kanuni za bunge, na uchaguzi wote ulikuwa na kasoro.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post