BABU WA MIAKA 71 AKAMATWA NA POLISI KWA KUMBAKA MJUKUU WAKE WA MIAKA 9


Kamanda wa polisi mkoani Pwani, kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga, akizungumza na baadhi ya waandishi mkoani hapo. 
****

MZEE Athuman Ramadhan Njuila ,miaka 71 ,mkazi wa Mbwewe,Bagamoyo,mkoani Pwani anashikiliwa na jeshi la polisi, kwa tuhuma ya kumbaka mtoto wa miaka 9, mwanafunzi wa darasa la pili ambaye ni mjukuu wake.

Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari,Kamanda wa polisi mkoani Pwani, kamishna msaidizi mwandamizi, Onesmo Lyanga, alisema mzee huyo alifanikuwa kufanya ukatili huo baada ya kumrubuni mtoto huyo aingie ndani ya nyumba yake kusikiliza muungurumo wa mashine. 

Alieleza kuwa baada ya mtoto huyo kuingia ndani,mtuhumiwa alimsukumia kitandani na kuanza kumwingilia kimwili. 

"Baada ya kupata taarifa hizo, tarehe 24 Aprili mwaka huu,tulimhoji mama mzazi wa mtoto huyo ambaye alikiri kutokea kwa tukio hilo "alieleza kamanda Lyanga. 

Akisimulia mkasa huo,mtoto aliyefanyiwa ukatili huo alisema siku hiyo alifika kwenye nyumba ya babu na kumkuta akiwa na bibi yake baadaye bibi aliondoka na kumuacha akiwa na babu yake ndipo babu akaanza kumwingilia kimwili.

Tayari jeshi la polisi limekamata mtuhumiwa Njuila kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.

Na Mwamvua Mwinyi- Bagamoyo 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527