WEMA SEPETU AMTEMBELEA MBUNGE GODBLESS LEMA


Msanii wa filamu nchini Wema Sepetu ambaye hivi sasa amehamia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ametimiza hadi yake kwenda kuonana na Mbunge wa Arusha mjini Mhe. Godbless Lema ambaye amepata dhamana siku ya Ijumaa na kutoka gerezani.


Wema Sepetu juzi alisema atakwenda Arusha kuonana na Mbunge huyo ambaye amekaa ndani kwa zaidi ya miezi mitatu na kusema ni faraja kwao saizi kuona ametoka na kuja kuendeleza mapambano


"Ni faraja kwetu kwamba sasa umerudi mtaani kuendeleza mapambano, kwenye mapambano haya hautakuwa mwenyewe, mdogo wako Wema nitakuunga mkono mpaka kieleweke. For that sake, kesho (jana) i'll be in Arusha kuonyesha Solidarity" alisema Wema Sepetu


Baada ya Wema Sepetu kufanikiwa kuonana na Mbunge wa Arusha Gobless Lema amefunguka na kusema saizi anajisikia furaha na amani kuwa ndani ya chama hicho
"Finally Met my brother, aisee Chadema inanipa furaha mimi. Nina amani ya moyo... Ona Venye nacheka .... It was A Good Day...."aliandika Wema Sepetu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post