TUNDU LISSU ASOMEWA MASHTAKA MATANO YA UCHOCHEZI

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia kwa dhamana Mbunge Tundu Lissu aliyefikishwa mahakamani hapo na kusomewa mashtaka matano.


Lissu amesomewa Mashitaka matano(5) ambayo ni yale yale aliyofutiwa hapo awali kuhusu maneno ya Uchochezi kwenye Uchaguzi wa Dimani,Zanzibar.


Serikali imesema upelelezi umekamilika na ikaomba kesi ianze kusikilizwa leo.Lissu aliiomba mahakama isisikilize kesi hii leo ili akashiriki Uchaguzi wa TLS utakaofanyika kesho mkoani Arusha.


Mahakama imekubali maombi ya Tundu Lissu na kumwachia huru kwa dhamana ya milioni 10 ambapo tayari amekwishapanda ndege kuelekea jijini Arusha Kushiriki Uchaguzi huo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post