Tanzia: MWANDISHI WA HABARI CHANNEL TEN VALENCE ROBERT AFARIKI DUNIA

Valence Robert (kulia) enzi za uhai wake akiwa na rais mstaafu Jakaya Kikwete
Valence Robert (kulia)

Habari tulizozipata hivi punde ni kwamba Mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoa wa Geita Valence Robert amefariki dunia leo mchana Jumanne Machi 28,2017 nyumbani kwao kijiji cha Mgana Wilaya ya Misenyi Bukoba mkoani Kagera.Chanzo cha kifo chake bado hakijajulikana.Valence Robert pia alikuwa anaandikia gazeti la Tanzania Daima.Enzi za uhai wake,Valence Robert alikuwa anaripoti Matukio ya mkoani Geita katika Malunde1 blog.

Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Geita Daniel Limbe amethibitisha taarifa za kifo cha mwandishi wa habari Valence Robert.

Limbe ameiambia Malunde1 blog kuwa Valence Robert  hivi karibuni aliondoka mkoani Geita akiwa  anaumwa.

Hata hivyo inaelezwa kuwa Valence Robert alikuwa anaumwa ugonjwa usiojulikana.
Mazishi yanatarajiwa kufanyika kesho nyumbani kwao Misenyi.

Hivi karibuni Valence Robert na Joel Maduka walipigwa na askari polisi wakati wakiwatawanya wananchi kwenye maeneo ya stendi ya zamani Mjini Geita ambao walikusanyika kusalimiana na Waziri mkuu mstaafu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu Taifa ya  Chadema Edward Lowassa.

 Kupitia ukurasa wake wa Facebook,mkurugenzi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde...ameandika

Nilifahamiana naye mwaka 2011 nikiwa Mhariri Mkuu wa Habari Radio Faraja Fm Stereo,alikuwa ananitumia habari nyingi za mkoa wa Geita.Hata Nilipotoka Radio Faraja mwaka 2012 Kijana Valence Robert aliendelea kuwa rafiki yangu,alinipigia simu mara kadhaa,usiku na mchana…aliniambia “Kaka kuna stori nimekutumia kwenye email yako…icheki kisha itupie kwenye blog yetu ya Malunde1 blog”….wakati mwingine aliniambia “Kaka niko mbali na mtandao,kaa vizuri nikusimulie utaandika mwenyewe huku kuna tukio”,…..Aliniambia anaandikia Gazeti na Tanzania Daima na hata alipoanza kuripoti Channel Ten aliniambia ...
Hakuogopa hatari mbele ya habari aliyoitaka...Valence Hakusita kunitafuta kila alipofika Shinyanga mjini….Daah!! Kweli duniani tunapita tu tangulia mshikaji wangu Valence Robert…
Poleni sana kwa msiba familia ya Valence Robert,waandishi wa habari mkoa wa Geita na nchi kwa ujumla.
Daima ntakukumbuka jama yangu..R.I.P Kaka.

'' kamanda yaani mwili hauna nguvu kabisa, nikitembea hatua mbili naweza kudondoka nitumie nini kamanda ili nipate nguvu maana kesho kutwa nataka nije huko''hayo yalikuwa maneno ya aliyekuwa mwandishi wa chanel ten na gazeti la Tanzania daima mkoani geita, valence Robert nilipoongea naye jana(27/8/2017)usiku ambapo baada ya kuongea na daktari wangu aliniambia nimwambie atumie oral ambapo nilimpigia na kumpa maelekezo hayo. Usiku huo huo pia tuliongea na akadai mwili wake umeanza kupata nguvu baada ya kutumia oral, asa nashangaa dada ake kunipigia simu leo na kuniambia Robert wa kwanza kulia(pichani) akiwa na Rais mstaafu jakaya Kikwete, amefariki dunia. Kiukweli nimeamini sisi tu wapitaji tu. Tumuombee

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post