SENTENSI 52 ZA BOSI WA CLOUDS MEDIA RUGE MUTAHABA AKIELEZA JINSI MAKONDA ALIVYOVAMIA OFISI YAO USIKU AKIWA NA ASKARI WENYE SILAHALeo Jumatatu Machi 20,2017 mkurugenzi wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba ametoa ufafanuzi kuhusu Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kuvamia ofisi za Clouds Media Group usiku akiwa na askari wenye silaha wakati wa kipindi cha Shirika la Wambea Duniani (SHILAWADU)

Ninazo hapa sentensi zaidi ya 50 za Ruge hapa

Ruge: Alhamisi asubuhi tulikuwa na kikao na Kamati ya Maudhui TCRA walikuja kutupatia msasa kidogo, akaja Mkuu wa Mkoa Makonda

Ruge:Katikati ya kikao Makonda alitutembelea tukaongea mambo kadhaa tukaagana na watu wa TCRA

Ruge:Wakati natoka ofisini nilikutana na Makonda na Vijana wa SHILAWADU nikauliza kwema hapa nikajibiwa ni Story za kawaida tu.

Ruge:Nikiwa kwenye gari alinifata mmoja wa watangazaji wa kipindi cha SHILAWADU kuniambia kuhusu mwanamke aliyezaa na Gwajima.

Ruge: Nikawauliza hiyo story mna uhakika nayo mmeibalance mmempata Mchungaji Gwajima? nilimpigia Mkuu wa Vipindi Kerry kumuuliza

Ruge: Nilitoa maelezo kwa boss wa vipindi CloudsTV kuhusu kipindi kisichokuwa na maana sababu hakija balance na kisiruke hewani.

Ruge: Niliwambia SHILAWADU siku ya Alhamis mchana kuwa wasiirushe 'Story' bila kuongea na upande wa pili (wa Gwajima)

Ruge: Niliwambia Vijana wa SHILAWADU kuwa 'Story' kama ndiyo anayoisubiri RC basi ajue haitaenda hewani hata kwenye Social Media.

Ruge: Nilimueleza Kerry ambaye ni kiongozi awasiliane na Makonda kwamba video yake haitoruka hewani sababu haija balance

Ruge: Saa 10 Alhamisi nilipata Simu ya Gwajima kunieleza kuhusu kuwepo kipindi kinachomuhusu nikamueleza hiyo story haitoruka

Ruge: Ijumaa niliwasisitiza SHILAWADU kuwa kipindi kile kisirushwe kwa kuwa 'Story' haiko balanced.

Ruge: Ijumaa saa 5 kasoro usiku nilipigiwa simu kuwa RC Makonda alikuwa kaja ofisini akiwa na maaskari 6 wakiwa na silaha.

Ruge: Baadaye nilipata simu toka kwa Mkurugenzi Mtendaji Joseph Kusaga kwamba anapewa lawama na RC Makonda tumezuia kipindi chake

Ruge: Nilimpigia simu RC Makonda kumhoji kwanini aje ofisini na maaskari wenye silaha? Akauliza kwanini nimezuia kipindi kuruka?

Ruge: RC Makonda alikata simu, lakini nilipaniki nikiwazia hizo silaha walizokuja nazo ofisini. 

Ruge: Nilipata maelezo kutoka kwa Sam aliyekuwepo mapokezi akanieleza RC Makonda alikuwa anachukua kitu kwenye flash

Ruge: Kwa Mara ya kwanza Makonda anatuvunjia heshima sisi kama rafiki zake tulifanya kazi naye vizuri tangu akiwa Mkuu wa Wilaya

Ruge: Paul Makonda ambaye ni rafiki yetu ametukosea,huwezi kuja ofisini kwetu usiku na tena na mabunduki.

Ruge: Makonda ana namba zangu kwanini asinipigie,Paul alikuwa rafiki yetu tangu akiwa mkuu wa wilaya na mimi siwezi kukataa urafiki.

Ruge: Walipofika ofisini waliondoka na FLASH yenye kipindi.

Ruge: RC Makonda alisema "Bahati yenu" baada ya kujua kuwa waliokataa vijana wa SHILAWADU sio waliozuia kipindi isipokuwa mimi.

Ruge: Nilimwambia Mkurugenzi wa Clouds(Kusaga) kuwa RC alitukosea heshima; kulikuwa na haja gani aje na silaha na ni rafiki yetu?

Ruge: Ukweli hakuna aliyepigwa ila kulijengwa hofu kubwa kwa wafanyakazi wa Clouds Media. Si jambo dogo hili!

Ruge: Tusikwepe ukweli kuwa sisi Clouds Media kama chombo cha habari tuna wajibu wa ku-balance story. Sijawahi kulazimishwa story.

Ruge: Naomba nieleweke wazi hatuwezi kumuacha mtu akatupanda kichwani hii ni dharau kwangu nasimamia watu zaidi ya 200 asinidharau.

Ruge: Makonda alitaka stori iruke wakati haijabalance,mimi kama msimamizi mkuu wa vipindi nilikataa.

Ruge: Kuacha shughuli za kazi, Makonda amekuwa akija hapa Clouds kama rafiki. Ila kitendo cha kuja na walinzi kiliwashtua walinzi.

Ruge: Kama watanzania, hatutaki kuiona bunduki mitaani,Mimi sitaki kuona bunduki mtaani kwa maslahi ya vizazi vya kesho, bunduki ziwepo wanapolinda benki sio kwenye media.

Ruge: Sisi tuhukumiwe kama taasisi, wafanyakazi wetu wasitiwe hofu.

Ruge: Mimi sikuwekwa ndani, nilienda Polisi kuripoti suala hili.

Ruge: Vijana wa SHILAWADU wapo kwenye hofu wametishwa wamepoteza morali na kazi yao hawana Amani tena wameomba likizo.

Ruge: Sisi Clouds Media tumeumia sana kwa haya aliyofanya Makonda,We want Respect,we want Heshima tu.

Ruge: Mtu akikosea kabla hatujaangalia cheo chake, tuangalie makosa yake. Si kudai eti wanaomkosoa wanapingana Vita ya Dawa za Kulevya.


Ruge: Sisi tuna namna yetu ya kuadhibiwa tunahitaji kuwe na Uhuru wa habari, sio kwakua una mamlaka fulani ukatupanda kichwani

Ruge: Mtu kuwa na nafasi ya Uongozi flani si sababu ya 'kuwapanda' watu . All we want is RESPECT!

Ruge: Ishu imetokea Ijumaa niliamini Makonda atakuja kuomba radhi Jumamosi.

Ruge: Mimi namlaumu kwa kitendo alichofanya,kwanza alikua rafiki,kwanza ni mkuu wa mkoa,urafiki wa mtutu hauhitajiki.

Ruge: Video clips za CCTV zinazozunguka mtandaoni kweli ni za hapa Clouds Media. Sisi tulidhani Makonda angeomba radhi kwa kadhia hii

Ruge:Suala ni kwamba tulifikiri ni mapungufu ya kibinadamu ina maana Makonda hakujua kuna Camera kila mahali, jambo la kutafakari

Ruge: Jumamosi tulidhani anaweza kuomba radhi, na kwenye mitambo ya CCTV kila mtu anapafahamu.sijui kaachia nani zile video, Ni kweli tuna Cctv kila sehemu maana hili ni jengo la habari 

Ruge: Makonda ni mdogo wangu sana anaweza kuniomba msamaha, akumbuke mimi nawakilisha kundi la watu waliokosewa kwenye hili.

Ruge: Niseme, urafiki na BUNDUKI siutaki. Wanaodai Makonda alikuja hapa Clouds akiwa rafiki wanapotosha!

Ruge: Viongozi wetu wanapenda kumtaja Mungu lakini matendo yao ni tofauti watu wanaumia kwenye hili 

Ruge: Kitu kibaya ambacho kinaumiza moyo RC Makonda ametumia vibaya madaraka yake pamoja na urafiki wake kwetu kama Media

Ruge; Tukiongea kwa watu wanasema tunahitaji mtu atumbuliwe lakini sisi tunaongea kwa nafasi yetu tumeumia kwenye hili 

Ruge: Clouds inalaani kilichotokea, na inaomba vyombo vya Habari vitoe ushirikiano katika kukemea hili.

Ruge: Kikubwa hatutaki kutengeneza hali yoyote ya kuyumbisha serikali,hatutaki kugombana na serikali. 

Ruge: Hatua ya maamuzi yetu bado tupo kwenye mashauriano hatutaki kupingana na ajenda za serikali kwa sasa, tutaamua cha kufanya.

Ruge: Tulikuwa tunaonekana hiki ni kitu cha Makonda lakini viongozi wengi hawatumii fursa wenye ajenda ya maendeleo waje hapa
Ruge:Sisi sio viongozi ni wananchi tuna miaka 20 kama chombo cha Habari tunakaribisha agenda zenye ubunifu, tujadiliane pamoja.

Ruge: Sisi kama Clouds Media tumeumia kuona tukio hili limetokea tena kwa mtu wetu ambaye angeweza kuhoji kwa njia nzuri 

Ruge:Tusimpe kazi ngumu Rais, huyu baba anatakiwa kuangalia maendeleo yetu, nimesema leo niongelee hili tuendelee na kazi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post