MWANDISHI NGULI DOTTO BULENDU AWACHAMBUA KIAINA NAY WA MITEGO,KASSIM MAJALIWA NA RAIS MAGUFULI


Toka jana,msanii Ney wa mitego,amevuma na kuteka vyombo vya habari kuanzia Tandahimba mpaka Washington,akapaa mpaka London na Bonn kwenye vyombo vya habari vya kimataifa!.

Ney wa Mitego leo katamba kurasa za mbele za magazeti ya Tanzania kuanzia yale ya udaku mpaka magazeti "serious",ya Kiswahili mpaka ya Kingereza,Kurasa za mbele ni habari na picha ya Ney wa Mitego!.

Ney wa Mitego,jana alikuwa ndiyo habari kuu kwenye matangazo ya jioni ya idhaa ya kiswahili ya BBC kwenye matangazo ya dira ya dunia(Radio),Ney wa Mitego alisikika Bonn DW-KISWAHILI,akawa kwenye habari tatu kuu za kwanza,Ney huyu alifanikiwa kupenya mpaka kwenye matangazo ya taarifa ya habari ya TV ya dira ya dunia ya BBC,akawa habari yenye uzito iliyoandaliwa kwa msingi wa 5W+H+W,badala ya 5W+H kama ilivyokuwa kwa habari nyingine!.

Ney hii leo kwenye baadhi ya magazeti ya Tanzania amepewa uzito kuliko Ripoti ya Faru John,Ripoti ya CAG(pitia gazeti la Mtanzania na Tanzania Daima),Nei kashindwa kupenya kwenye magazeti ya serikali pekee(Habari leo na Daily news) ila akapamba kurasa za michezo za magazeti hayo?

Ney wa Mitego,leo kapata uzito sawa sawa na Rais John Magufuli na Waziri Mkuu Kasimu Majaliwa kwenye vyumba vya habari,(magazetini,redioni ,TV mpaka mitandaoni).

Je vigezo vilivyomuweka kurasa za mbele Ney ndiyo hiyo hivyo vuilivyotumika kwa Rais Magufuli na Kasimu Majaliwa,kuanzia redio za Tandamba mpaka Bonn,Washingtin Na London?

1.Ney kapata nafasi na ukipaumbele kutokana na kuzingatiwa kwa kigezo cha takwa na hitaji la walaji(audience needs and wants),jana mitandaoni,mitaani watu walikuwa wakijadili saa kuhusu Wimbo wa Ney na kukamatwa kwake,mijadala hii iliipiku ripoti ya Faru John na ile ya CAG!.

2.Ney kihabari ni mtu maarufu(celebrity) wakati Magufuli na Kasimu Majaliwa ni "Prominent figures",kuwa celebrity na kuwa prominent figure kote kuna kupa nafasi ya kutengeneza habari!.

3.Ney kakaa ukurasa wa mbele baada ya kujiongezea sifa mbili za habari,Unusul(jambo kutokuwa la kawaida)na "impact",Ney,anatoa wimbo,Polisi wanamkamata,Basata wanaufungia,Rais anajitokeza na kutupilia mbali maamuzi ya Polisi na Basata,maamuzi ya Raisi yaliiongezea uzito story ya Ney,!

4.WewaSepetu alipoondoka CCM na kujiunga na CDM aliweza kuteka kurasa za mbele ya magazeti ya kiswahili ila hakupenya kwenye kurasa za mbele za magazeti ya kingereza,jana Ney alikuwa anashindana na Rais Magufuli,Waziri mkuu Majaliwa kukaa ukurasa wa mbele wa magazeti.Wema yeye alihama tu,na hata alipokuwa anahama hakupatwa na jambo lolote ambalo lingeongeza uzito wa habari yake,alibaki kubebwa na sifa ya kuwa maarufu akatengeneza habari,lakini Ney,ana umaarufu,anakamatwa,Rais anasema mwachieni,na wimbo wake pigwe mnooo,hapo Ney anajiongezea alama za kutengeneza habari.

Rais kuna sehemu kashindwa kumuondoa kileleni Nay kutokana na Ripoti yake kutoainisha maudhui zaidi ya kukabidhiwa tu huku ikiwa na dhana kama mbili tu,story ya CAG nadhani itapata mshindo huko Dodoma wakati wabunge watakapoijadili.

Suala la Faru John,ni kama limekwisha vile,media imeriripoti kikawaida,ukiitazama story ya Ney kwa jicho la tatu,inabebwa na dhana nne(timely,impact,celebrity na unusual),story ya Raisi ana Waziri Mkuu inabebwa na dhana mbili(Prominency,Timely)

Rais Magufuli yeye kapiga hodi kupewa nafasi kuwa habari kuu kwenye magazeti ya Habari leo na Daily news ambayo kiitifaki,yeye ndiye mhariri mkuu,ila kivitendo siye mhariri mkuu,waziri mkuu Majaliwa kapiga hodi na kupewa nafasi kwenye magazeti ya Nipashe na The Guardian,huku Ney akitamba Tanzania Daima na Mtanzania huku magazeti mengine yakimpa nafasi pia kurasa za mbele!.

Gazeti la Mwananchi lenyewe limetafuta upekee,habari kuu limempa Waziri Mwigulu,walichokifanya Mwananchi kuendeleza dhana ambayo ipo sana kwenye vyombo vya habari vya Magharibi,dhana ya "New developing story",wao wameendelea kuifuatilia habari ya aliyemtolea bastola Nape Nnauye!.

Mwananchi hawajataka kuondoshwa kwenye njia ya kuujua ukweli juu ya aliyemtishia bastola Nape,Ney,Faru John na CAG RIPOTI,zimeshindwa pata nguvu dhidi ya ukweli kuhusu aliyemtishia Nape bastola!

Mwananchi wameipima habari kuu yao kwa kuzingatia msingi wa "NEW DEVELOPING STORY",wakati magazeti mengine yote nchini yamezingatia msingi wa jambo jipya na lenye mshindo huko mtaani(5w+H).

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post