MBUNGE ALIYEFUNGWA JELA KWA VURUGU WAKATI WA UCHAGUZI AACHIWA HURU


January 11 2017 Mbunge wa Kilombero kwa tiketi ya CHADEMA Peter Lijualikali alihukumiwa miezi 6 jela baada ya kupatikana na hatia katika kesi ya kufanya vurugu kipindi cha uchaguzi wa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero. Mbunge Lijualikali alishitakiwa kwa kuwashambulia polisi kwenye siku hiyo ya uchaguzi.

Leo Machi 30 2017 Mahakama kuu kanda ya Dar es salaam imetengua hukumu hiyo iliyotolewa na mahakama ya wilaya ya Kilombero, sasa Mbunge huyo amechiwa huru.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post