MAKAMISHNA WAPYA WA UHAMIAJI WAAPISHWA DODOMA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira aliyeketi katikati akishuhudia Makamishna wapya wa Uhamiaji wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma baada ya kuvishwa vyeo vipya katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba Yahaya na kushoto ni Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala wote wakishuhudia tukio hilo.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala ,akimvisha cheo kipya Kamishna wa Uhamiaji Utawala na Fedha, Edward Peter Chogero katika hafla iliyofanyika jana katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Anayeshuhudia ni Naibu Kamishna wa Uhamiaji Chrispin Ngonyani. Tukio hili linehudhuriwa na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba Yahaya.
Kamishna mpya wa Uhamiaji Divisheni ya Sheria Hannerole Morgan Manyanga akila kiapo cha Utii mbele ya Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dr. Anna Peter Makakala katika hafla iliyofanyika  katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Balozi Hassan Simba Yahaya.
Kamishna wa Tume ya Maadili ya Utumishi wa Umma , Jaji Mstaafu Harold Nsekela wa kwanza kushoto akiwaongoza Makamishna wapya wa Uhamiaji kuapa kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma baada ya Makamishna hao wapya kuvalishwa vyeo vipya katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Makamishna wapya wa Uhamiaji wakisaini Fomu za Maadili ya Viongozi wa Umma baada ya Makamishna hao kula kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Utumishi wa Umma, katika hafla iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Meja Jenerali Projest Rwegasira akitoa maelekezo kwa Makamishna wapya wa Uhamiaji wakati wa hafla ya kuvikwa Vyeo Vipya iliyofanyika leo katika ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Meja Jenerali Projest Rwegasira akizungumza jambo na Makamishna wapya wa Uhamiaji baada ya kumalizika shughuli ya kuapishwa Makamishna hao leo katika viwanja vya Ofisi ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post