LOWASSA AMTAKA RAIS MAGUFULI KUFUTA KAULI YAKE

Image result for lowassaAliyekuwa Waziri Mkuu na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Edward Lowassa, amemtaka Rais Dkt. John Magufuli kuifuta kauli yake ya kuwataka wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wasishirikiane na wabunge wa vyama vya upinzani.

Alizungumza hayo jana kwenye ziara ya viongozi wa CHADEMA katika mkoa wa Pwani na Dar es Salaam. Lowassa alidai kuwa kauli hiyo ya Rais Dkt. Magufuli inabomoa misingi ya amani iliyowekwa na waasisi wa taifa letu. 

Alisema “Namuomba Rais aisahihishe kauli hiyo na nawaomba watanzania tukatae kugawanywa… Tusikuballi, nchi hii ni yetu sote hakuna mtu mwenye haki miliki hapa. Ikienda vibaya tutaangamia wote na ikienda vizuri tutafaidi wote, kwahiyo tukatae.”

Aliongeza kuwa watanzania wamekuwa wakiishi bila kubaguana kwa misingi ya dini, rangi au ukabila na kukumbushia kauli iliyowahi kutolewa na baba wa taifa kuwa ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukishakula hutotaka kuiacha.

Katika kikao hicho alizungumzia pia juu ya hali ya maisha na uchumi kuwa mgumu, bei za bidhaa kupanda  na mipango mibovu ilivyosababisha sekta binafsi kuyumba hali iliyosababisha kuongezeka kwa watu wasio na ajira nchini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post