HII NDIYO NCHI AMBAYO UKIKAMATWA UNAENDESHA GARI UMELEWA...UNAPELEKWA CHUMBA CHA KUHIFADHI MAITI

Tanzania, Kenya , Uganda , Rwanda na hata Burundi utaona mabango makubwa yamewekwa kando ya barabara kuonya madereva kuto endesha magari wakiwa wamelewa.

Mabango hayo mbali na kukutishia kwamba unaweza kufariki kutokana na ajali, pia yanaonya kwamba ukipatikana utatozwa faini kubwa kama njia ya kukutia adabu kwa kosa la kuendesha gari ukiwa mlevi.

Lakini nchini Taiwan mambo ni tofauti kabisa,Dereva yeyote anayepatikana na kosa la kuendesha gari akiwa mlevi , anakamatwa na kupelekwa kwenda kufanya kazi katika chumba cha kuhifahdi maiti.

Mkuu wa mashtaka katika jimbo la Taitung huko Taiwan, amedai kwamba madereva wanaopatikana na kosa la kuendesha gari wakiwa wamelewa wanapewa kazi maalum ya kusafisha meza za kuwa pasulia maiti. Na pia wanatakina kuosha na kusafisha kabisa friji za kuwekea maiti.

Sababu kubwa hasa ya kufanya hivyo ni kuwapa madereva hao fursa ya kuona maiti hasa zile zitokanazo na ajali za barabarani jinsi zilivyo pondeka pondeka zinapoletwa na hata kutolewa kutoka hizo mochwari.

Wakuu wa mashtaka wanatarajia kwamba pengine fursa ya kuona maiti hizo zitawafunza jinsi gani maisha ni muhimu na ni sharti ya heshimiwe kwa dereva kuwa waangalifu barabarani na kuepuka na tabia ya kuendesha gari ukiwa umelewa.

Badala ya watu kupinga adhabu hiyo, sasa mitandao ya kijamii imejaa kauli za watu wakisema badala ya kupanguza tu meza za upasuaji maiti pamoja na friji za kuwekea maiti hizo.

Ukipatikana na kosa la kuendesha gari ukiwa umelewa bora upewe adhabu ya kuosha maiti , tena maiti za watu waliofariki kutokana na ajali za barabarani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post