WATUHUMIWA WA DAWA ZA KULEVYA WAKIFIKISHWA MAHAKAMANI..WAMO WASANII


Takriban watuhumiwa 10 wa dawa za kulevya ambao ni miongoni mwa watu waliotajwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo asubuhi.

Miongoni mwa waliofikishwa mahakamani sasa ni wasanii Rommy Jones, TID, Babuu wa Kitaa, Petit Man, Tunda (model wa kike), Lulu Diva, Recho, Joan, na wengine.

Watuhumiwa wote wamesomewa kiapo cha Mahakama ambapo upande wa Jamuhuri umeomba watuhumiwa hao waamrishwe kuwekwa chini ya uangalizi kwa kuripoti polisi mara 2 kwa mwezi kwa kipindi cha miaka 2 ili kuangaliwa kama wameacha tabia ya kutumia dawa hizo hususani bangi

Wakili wa upande wa utetezi amedai taarifa hizo hazijakamilika kwani hazioneshi wanaojiusisha na dawa za kulevya na walikamatwa lini na wapi na hakuna ushahidi wa kujitosheleza wa madai hayo kiasi cha wao kupata dhamana ya kuangaliwa tabia zao bila polisi kutoa ufafanuzi wa kina wa kwanini wanahitaji kupata dhamana ya uangalizi wa nidhamu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post