Picha 20: KIKAO CHA PACESH,WASAIDIZI WA KISHERIA WAPATIWA LAPTOP SHINYANGA VITA DHIDI YA UKATILI WA KIJINSIA

Ijumaa Februari 10,2017 kumefanyika kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Elimu Kwa Watoa Msaada wa Kisheria katika wilaya ya Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga.

Kikao hicho kilichoandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Paralegal Aid Centre Shinyanga (PACESH) linalohusika na utoaji wa msaada wa kisheria kimefanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa wilaya ya Shinyanga.

Akizungumza katika kikao hicho mgeni rasmi,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga alipongeza jitihada zinazofanywa nan a PACESH katika kupinga ukatili wa kijinsia na kusisitiza kuwa serikali inatambua uwepo wao na itaendelea kuwaunga mkono katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia.

“Kazi yenu ni nzuri,kinachotakiwa sasa ni kuongeza kasi ya utoaji elimu kwa wananchi ili wajue haki zao ili wanapopata matatizo wajue nini cha kufanya”,alieleza Matiro.

Aidha alisema elimu kuhusu haki za wananchi pia inatakiwa kutolewa kwa viongozi wa serikali za mitaa kwani kama viongozi watakuwa na uelewa wa kutosha itasaidia kumaliza tatizo la ukatili wa kijinsia.

“Bado watoto wanabakwa,wanapewa ujauzito,wanawake wanapigwa,wananyimwa haki zao,ili tuweze kumaliza tatizo la ukatili wa kijinsia ni lazima wadau wote waungane,bila ushirikiano hatuwezi kumaliza tatizo hili”,aliongeza Matiro.

Kikao hicho mbali na kujadili masuala mbalimbali yanahusiana na ukatili wa kijinsia pia jumla ya kompyuta mpakato (laptop) sita zimekabidhiwa kwa wasaidizi wa kisheria katika vituo vya usaidizi wa kisheria mkoani Shinyanga.

Kompyuta hizo zimetolewa na shirika mama la Usaidizi wa Kisheria la Legal Service Facility (LSF) la lenye makao makuu yake jijini Dar es salaam.

Akizungumzia kuhusu kompyuta hizo,Meneja Miradi wa shirika la PACESH John Shija alisema zimelenga kusaidia katika shughuli za kiutendaji katika vituo vya usaidizi wa kisheria.

Tazama picha 20 za matukio wakati wa kikao hicho..Picha zote na Kadama Malunde -Malunde1 blog
Mgeni rasmi katika kikao cha Tathmini ya Utekelezaji wa Mradi wa Kupinga Ukatili wa Kijinsia na Elimu Kwa Watoa Msaada wa Kisheria katika wilaya ya Shinyanga na Kishapu mkoani Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akizungumza katika kikao hicho cha wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia wilaya ya Shinyanga na Kishapu ambapo aliwataka wananchi kuwa wanajitokeza kutoa ushahidi katika kesi kutokana na kuwepo taarifa kuwa kesi nyingi zimekuwa zikishindwa kuendelea kutokana na ushahidi kukosekana.
Mkurugenzi wa shirika la PACESH Perpetua Magoke akizungumza wakati wa kikao hicho ambapo alisema shirika lake limekuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa mkoa wa Shinyanga dhidi ya ukatili wa kijinsia
Mkurugenzi wa shirika la PACESH Perpetua Magoke alitumia fursa hiyo kuwataka wananchi kutokuwa waoga kuwafichua watu wanaofanya ukatili dhidi ya wanawake na watoto kwani kukaa kimya kunasababisha vitendo vya kikatili kuendelea kujitokeza katika jamii
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la PACESH,Mchungaji Paul Mpanda akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ni wakati mzuri sasa wananchi wakabadilika na kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili vinavyofanyika katika familia zao na jamii kwa ujumla
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la PACESH,Mchungaji Paul Mpanda akisisitiza jambo ukumbini
Meneja Miradi shirika la PACESH John Shija akielezea kuhusu mradi wa Kuimarisha Uendelevu wa wasaidizi wa kisheria katika wilaya za mkoa wa Shinyanga
Meneja Miradi shirika la PACESH John Shija akiendelea kuelezea kuhusu mradi wa Kuimarisha Uendelevu wa wasaidizi wa kisheria katika wilaya za mkoa wa Shinyanga
Meneja Miradi shirika la PACESH John Shija alisema miongoni mwa malengo ya mradi huo ni kuongeza upatikanaji wa huduma bora ya msaada wa kisheria katika jamii mpaka kufikia mwaka 2021
Malale Johola kutoka Dawati la jinsia wilaya ya Shinyanga akielezea namna dawati hilo linavyoshughulikia kesi mbalimbali zinazohusu ukatili wa kijinsia dhidi ya watoto na wanawake
Malale Johola kutoka Dawati la jinsia wilaya ya Shinyanga akiendelea kutoa taarifa
Mwenyekiti wa dawati la jinsia na watoto wilaya ya Kishapu Rose Mbwambo akitoa taarifa kuhusu masuala ya ukatili wa kijinsia ambapo alisema kesi nyingi zimekuwa zikifutwa kutokana na kukosekana kwa ushahidi hali inayosababisha vitendo vya ukatili viendelee kujitokeza katika jamii
Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka PACESH Pendo Mgeta akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema bado jamii haijawa na uelewa kuhusu haki zao huku akiitaka jamii kuacha uoga kuwafichua wahusika wa vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto
Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka PACESH Pendo Mgeta 
Wadau wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro(kulia) akimkabidhi Kompyuta mpakato bwana Buyamba Ngogeja kwa niaba ya wasaidizi wa kisheria katika kituo cha usaidizi wa kisheria wilaya ya Kishapu.Laptop hizo zimetolewa na shirika mama la Usaidizi wa Kisheria la Legal Service Facility (LSF) la lenye makao makuu yake jijini Dar es salaam.
Wasaidizi wa kisheria katika kituo cha usaidizi wa kisheria wilaya ya Shinyanga wakipokea laptop.Aliyevaa suti kushoto ni bwana Deogratius Kashindye akishikana mkono na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la PACESH,Mchungaji Paul Mpanda 
Bi Sophia Malimo kutoka Manispaa ya Shinyanga akipokea laptop kwa ajili ya kituo cha usaidizi wa kisheria wilaya hiyo
Bi Sophia Malimo kutoka Manispaa ya Shinyanga akishikana mkono na meneja miradi kutoka PACESH John Shija wakati akipokea laptop

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post