RAIS MAGUFULI AMTEUA JENERALI VENANCE MABEYO KUWA MKUU WA MAJESHI YA ULINZI TANZANIAJenerali Venance Mabeyo

Rais John Magufuli amemteua Luteni Jenerali Venance Mabeyo kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Taarifa ya Ikulu jijini Dar es Salaam imesema pamoja na kuteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Luteni Jenerali Mabeyo amepandishwa cheo na kuwa Jenerali.

Jenerali Mabeyo anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Davis Mwamunyange ambaye amestaafu.

Wakati huo huo Rais Magufuli amemteua Meja Jenerali James Mwakibolwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Taarifa hiyo imesema pamoja na kuteuliwa kuwa Mnadhimu Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Meja Jenerali Mwakibolwa amepandishwa cheo na kuwa Luteni Jenerali.

Luteni Jenerali Mwakibolwa anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jenerali Mabeyo ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post