JINSI MANJI ALIVYOTUA POLISI BAADA YA KUTAJWA KUHUSIKA DAWA ZA KULEVYA

Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha Polisi cha Kati leo saa 4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi.

Manji amefika leo badala ya kesho ambapo yeye na wengine 64 walitakiwa kufika kituoni hapo.

Manji ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na waandishi wa habari na kusema hatoweza kufika kituoni hapo siku ya Ijumaa.


Amewasili leo na gari aina ya Range Rover rangi nyeusi .

Manji amefika kituoni hapo akiwa na wanasheria wake 8 ambapo wanasheria 6 ni raia wa Tanzania na wanasheria wawili ni raia wa Uingereza.

Aidha, mashabiki wa Yanga wamejitokeza kwa wingi kituoni hapo kumuunga mkono kiongozi wao.

Mbali na Manji, wengine waliotajwa katika orodha hiyo ni Pamoja na Fremaan Mbowe, Askofu Josephat Gwajima, Iddi Azan. Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post