IRENE UWOYA ANA MPANGO WA KUWA MCHUNGAJI KWENYE KANISA LAKE


Msanii wa filamu Irene Uwoya amesema kuwa ana mpango wa kuwa Mchungaji pamoja na kumiliki kanisa lake yeye mwenyewe siku za usoni na kwamba anamuomba Mungu kila siku aweze kutimiza ndoto hizo.

Kauli hii imetoka kinywani mwa msanii huyo pindi alipokuwa akijibu maswali mubashara aliyokuwa anaulizwa na mashabiki zake kupitia katika ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipindi cha Kikaangoni

"Nina ndoto ya kuwa mchungaji na kila siku huwa nina muomba Mungu anifanikishie suala hilo niweze kutimiza japokuwa sasa hivi bado nipo katika changamoto kubwa ila natumai ndoto zangu zitatimia. Natamani kuwa pastor ambaye ni mwalimu, niwafundishe watu Mungu anataka nini, lakini sitaki kuanzisha kanisa kama biashara, sitaki kucheza na Mungu, ndiyo maana najipanga kwanza sitaki kukurupuka, nataka niwafundishe watu Mungu anataka nini, na jinsi ya kumuomba Mungu". Alisema Uwoya

Uwoya pia amefunguka na kueleza kuwa kazi yake ya sanaa huwa inamtesa kiimani jambo ambalo linamfanya kila siku akiamka awe anatubu kwa ajili ya mambo anayoyafanya akiwa katika kazi zake za uigizaji .

Amesema katika tasnia ya uigizaji mara nyingi huwa wanaongea uongo na hata mambo mengi wanayoyafanya kufikisha ujumbe huwa ni vitu ambavyo havimpendezi Mungu.

"Mimi nina hofu ya Mungu sana pia napenda kusali linapokuja suala la kazi yangu ukweli naona kama inanisumbua imani yangu kwa sababu katika uigizaji mambo mengi tunayoyafanya siyo ya kumpndeza Mungu lakini ndiyo kazi sasa, kila siku asubuhi nikiamka huwa inabidi kumuomba msamaha mungu wangu ndiyo niendelee na kazi". Amesema Irene Uwoya.

Kwa waliotaka kujua kama Irene anatumia dawa za kulevya, amewajibu kuwa hatumii dawa za kulevya na hajawahi kutumia kwa kuwa ni mkristo na dini yake hairuhusu kutumia dawa za kulevya wala kushiriki katika ndoa za jinsia moja lakini pombe anakunywa

"Situmii dawa za kulevya lakini nakunywa bia, dini yangu haizuii kunywa, nina uwezo wa kumaliza hata kreti nzima, hata mapadre kwenye dini yetu wanakunywa, lakini hairuhusiwi kulewa"

Pia amefunguka kuhusu mapenzi yake ya kuvaa nguo fupi, ambapo amesema anapeda nguo fupi, kwa kuwa ana mzio 'allergy' na nguo ndefu, hivyo hawezi kuvaa nguo ndefu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post