BUNGE LASIMAMA BAADA YA PAA LA JENGO LA BUNGE KUNG'OLEWA NA UPEPOShughuli za ukarabati zinaendelea kwenye jengo ya bunge nchini Ghana baada ya upepo mkali kung'oa sehemu za paa la jengo hilo siku ya Jumanne jioni wiki hii.

Kisa hicho kilisababisha kusitishwa vikao kwa ghafla wakati mvua ilipoanza kunyesha ndani ya jengo kutokana na paa hilo kung'olewa na upepo.

Wafanyakazi walijaribu kukinga baadhi ya maeneo yaliyoachwa wazi kwa kukusanya maji wakitumia ndoo.

Jengo hilo lililo kwenye mji mkuu Accra lilikarabatiwa miaka miwili iliyopita.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post