Video: KONDAKTA WA DALADALA ADAIWA KUUAWA KWA KUSHAMBULIWA NA WANAJESHI TANGA

Kondakta wa daladala linalofanya safari zake kati ya Nguvumali hadi Raskozone, Salim Kassim amefariki dunia baada ya kudaiwa kushambuliwa ndani ya kambi ya jeshi jijini Tanga.



Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Benedict Wakulyamba, kondakta huyo alikufa wakati akipelekwa katika Hospitali ya Mkoa ya Bombo na chanzo cha kifo bado kinachunguzwa.


Imeelezwa kuwa tukio hilo lilitokea juzi usiku, ambapo mashuhuda walidai kuona kondakta huyo akichukuliwa na wanajeshi na kuingizwa kambini na baadaye alitolewa akiwa hajitambui


Akizungumzia tukio hilo, Khalid Juma mkazi wa Nguvumali jijini hapa alisema askari hao wamekuwa na desturi ya kuwapiga wananchi bila kuchukuliwa hatua zozote za kisheria.


“Tumekuwa tukipata vipigo kila wakati, licha ya viongozi kupata taarifa za matukio hayo wamekaa kimya na hili tukio ni la tatu kutokea hapa,” alidai Khalid.


Diwani wa Kata ya Nguvumali ambaye pia ni Meya wa Jiji la Tanga, Alhaji Mustapha Selebosi alisema sababu za kipigo hicho ni mwanafunzi wa shule moja jijini Tanga ambaye ni mtoto wa ofisa wa JWTZ kuzozana na kondakta.

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527