UNDER THE SAME SUN YATOA ELIMU KWA WADAU KUHUSU UALBINO JIJINI MWANZA


Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mwanza Isaac Ndassa, akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, kwenye ufunguzi wa semina kwa wadau wanaosaidia kutokomeza ukatili dhidi ya watu wenye ualbino, inayofanyika kwa siku nne kuanzia leo Jijini Mwanza. 

Semina hiyo imeandaliwa na Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun ambapo imelenga kupanua uelewa kwa wanajamii/ wadau kuhusu ualbino ili kusaidia kupambana na ukatili kwa watu wenye hali hiyo.
Muasisi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualbino la Under The Same Sun, lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash, akizungumza na wanahabari kwenye semina hiyo.
Mkurugenzi wa Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualibino la Under The Same Sun nchini Tanzania, Bi.Vicky Ntetema, akifafanua jambo kwenye semina hiyo.
Mkufunzi Dr.George Rhoades kutoka nchini Marekani, akisisitiza jambo 
*******
Shirika la kimataifa la kutetea haki za watu wenye ualbino duniani, Under The Same Sun, limebainisha kwamba vitendo vya ukatili dhidi ya watu wenye ualibino nchini vinaendelea kupungua.

Mkurugenzi wa shirika hilo nchini, Vicky Ntetema, ameyasema hayo leo Jijini Mwanza kwenye semna kwa wadau wanaofanya kazi kwa ukaribu na watu wenye uaribino kutoka taasisi mbalimbali ikiwemo za kijamii, elimu na afya.

Ntetema amesema elimu inayoendelea kutolewa kwa wanajamii imesaidia kupunguza ukatili kwa watu wenye ualibino ikiwemo kukatwa viungo na mauaji licha ya kwamba kumekuwepo taarifa za makaburi ya watu wenye ualibino waliofariki kufukuliwa katika mikoa ya Kagera, Mbeya na Morogoro.

Mwasisi wa shirika hilo lenye makao yake makuu nchini Canada, Peter Ash, ameeleza kufurahishwa na maendeleo ya wanafunzi zaidi ya 300 wenye ualibino wanaosomeshwa na shirika hilo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa ambapo amewasihi wanajamii kuondokana imani potofu juu ya watu wenye ualibino ili kutokomeza ukatili dhidi yao.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Afisa Maendeleo ya Jamii mkoani Mwanza Isaac Ndassa, amesema serikali imelenga kuhakikisha vitendo vya ukatili kwa watu wenye ualibino vinatokomezwa ambapo amesisitiza elimu zaidi kuendelea kutolewa kwa wananchi ili kufanikisha lengo hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post